Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amezungumzia video aliyorekodiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare na kusema ni ya kutungwa na vyombo vya dola.
Video iliyozua utata hiyo hapo juu.
Dk. Slaa pia amelituhumu Jeshi la Polisi kufanya mchezo mchafu kwa maslahi ya kisiasa.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho kufafanua suala la kushikiliwa kwa Lwakatare.
Dk. Slaa, alilalamikia jeshi la polisi kuwa limekuwa likitumika kisiasa huku akitoa mfano wa chama hicho kuwa kimekuwa kikitaarifu jeshi la polisi kuhusu mambo hayo lakini halijawahi kuchukua hatua.
Alisema jeshi la polisi halijawahi kuchukua hatua stahiki kwa suala la mauaji ya Daudi Mwangosi kumwajibisha Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa aliyesimamia na kufanikisha kifo cha mwandishi huyo wa habari, jeshi la polisi pia halikuchukua hatua za kumhoji Dk. Stephe Ulimboka baada ya kuteswa na mtu anayedaiwa kuwa ni Afisa wa usalama wa Taifa wa Ikulu, hali kadhalika hawezi kushangaa ikiwa jeshi la polisi halitaacha kumhoji Absalom Kibanda.
Amesema, jeshi la polisi limekuwa likitoa taarifa za kukichafua chama, akikumbushia suala la Mwangosi, alisema kuwa mara tu baada ya tukio la Mwangosi kuuawa, jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wake lilitoa taarifa kuwa alilipuliwa na kitu kilichorushwa kwake akikimbilia kujisalimisha kwa polisi akitoka kwa wafuasi wa Chadema, jambo ambalo lilikuwa sio kweli.
Hivyo alisema, Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Chama hicho kuhusishwa kwa sakata la sasa la mkanda wa video uliopo katika mtandao na Kibanda ni mwendelezo tu wa kukihujumu chama, unaoratibiwa na Usalama wa Taifa, huku ukitekelezwa na jeshi la polisi.
“CHADEMA kinafahamu kwa undani, kwamba uzushi huu wa Tape ya “Bukoba Boy”.Tunajua huu umeanzishwa na kuhusisha Usalama wa Taifa, akiwemo Ighondo na wenziwe pale Ada Estate. Huyu Ighondo ambaye anafahamika pia kwa jina la “Rama” tunamfahamu vizuri sana," alisema.
Dk Slaa aliingiza suala la kufungiwa suala la kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi akiituhumu serikali kutokua makini.
Akakumbushia kuwa waliwahi kutuma barua mbalimbali polisi zinazothibitisha kuwa wanafanyiwa michezo michafu huku zikiwa zimeandikwa majina ya viongozi wa CHADEMA, au taarifa za Vikao vya Chadema zilizopotoshwa lakini polisi hawakuchukua hatua.
Aliongeza kuwa wakati wa uchaguzi wa Igunga walisema kuwa kuna mtu anamiliki bastola isisvyo halali, wakataja hadi namba za bastola iliyoingizwa lakini polisi hawajawahi kushughulika nayo.
Hata hivyo alishangazwa na jeshi la polisi kufanya haraka kumshikilia Lwakatare, kwani vyombo vya habari hivi majuzi vimemtaja kwa majina ya watu kuhusishwa na utekwaji na uteswaji wa Kibanda, lakini jeshi halikusema lolote hadi sasa.
Akaongeza kuwapo watu aliowataja kwa majina kwamba waliingia kwa ID zao kwenye mitandao kukejeli suala la kuteswa Absalom Kibanda lakini jeshi halikuchukua hatua.
Alishangazwa jinsi polisi walivyofanya haraka kumkamata Lwakatare, akasema ni mbinu tu za kukichafua CHADEMA.
Hadi tunaenda Mitamboni, Jeshi la polisi lilikuwa halijatoa taarifa kuwa Mkurugenzi huyo wa Ulinzi na usalama wa Chadema angepata dhamana au la, lakini Wakili wake alilithibitishia gazeti hili kuwa wameenda tena kumpekua kwa mara nyingine nyumbani kwake.
Kutokana na hali hiyo, Dk Slaa alisisitiza kuwa “madai yaliyotolewa mara nyingi na CHADEMA, kwa Rais kuandikiwa barua na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, iundwe Judicial Commission of Inquiry (Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza vifo vyote vyenye utata na sura ya kisiasa).
Akahoji ,Serikali inaogopa nini kuunda Tume hii huru ili ukweli Ujulikane? Iweje CHADEMA inayotuhumiwa Kupanga njama wanaishinikiza Serikali kuunda Chombo huru na Serikali ndiyo inayopata kigugumizi?”
Aliongeza kuwa “kwa wale walioumizwa na kujeruhiwa kama kina Ulimboka Kibanda na wengine, tunarudia Tamko letu la kuwa hatuna Imani na uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwa viongozi wa Jeshi hilo ni sehemu ya watu tunaowatuhumu kwa kuhusika kwa njia mbalimbali, na Ushihidi wa wazi na Taarifa mbili za Serikali kupingana yaani Taarifa ya Kamati yqa Nchimbi na Tume ya Haki za Binadamu.
"Tutaiaminije Polisi na Serikali kwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi? Hatuwezi kuendelea kuvumilia ukandamizaji huu wa uhuru wa habari, ambao sasa unaelekea kuota mizizi nchini kwetu. Na kweli ninawaomba na kuwataka waandishi wote msimame imara, bila kujadili itikadi, au tofauti zetu zozote zile na kusimamia uhuru wa Habari. Tunataka vivyo hivyo, kwa wanaharakati mbalimbali. Waache hofu, eti wanaogopa kuhusishwa na vyama vya Siasa! Haki ni haki na haina rangi ya bendera ya chama chochote," alisema.
Azungumzia Bunge:
Dk Slaa amesema kuwa usalama wa Taifa, unafanya kazi kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi hadi ndani ya bunge, ndio maana sasa wabunge wa Chama hicho wameondolewa katika kamati muhimu ambazo walikuwa wanazisimamia, bila wao kuulizwa, tofauti na walivyojaza katika fomu na nje ya ushauri wa Kiongozi wa upinzani bungeni.
Dk slaa alisema hiyo yote ni hujuma, Mnyika amepelekwa Ardhi maliasili na Mazingira, huku Msigwa akiondolewa maliasili na utalii kwa kuwa alikuwa anawataja viongozi wa CCM , jeshi la Polisi, jeshi la Wana nchina Ikulu yenyewe kuhusishwa na ujangili wa wanyama.
Amesikitishwa na wabunge wa Chama chake kuhamishwa kamati muhimu walizokuwa wanazisimamia, huku wengine wakiachwa kuingizwa katika kamati jambo ambalo linawanyima ufuatiliaji wa utendaji wa serikali, ilihali wabunge wengi wa CCM wengine wamewekwa kamati mbili kwa mbunge yule yule.
CHANZO: FIKRA PEVU
Comment
Comment by Joe Tesha on April 9, 2013 at 9:55am
ebhana kwel siasa ngum xanaaaaaaaa! cjui 2naelekea wap xaxa....!
Comment by fredrick mdassa on March 18, 2013 at 8:55pm tusiwe na haraka yakufanya justfication,hili siyo la wanasiasa,linahitaji utaalam unaojitosheleza.natuvute subira!
Comment by TɹAVELLER on March 17, 2013 at 12:54pm Huyu jamaa ni mchafu sana! KWA NINI HUTUMII TISSUE KUPENGA MAKAMASI, UNAFUTA MAKAMASI YAKO KWA VIDOLE HALAFU UNASHIKA PENI KISHA HIYO PENI UNAMPA MTU MWINGINE ANAITUMIA NA UNAJUWA MARA NYINGI BAADHI YA WATU WANA TABIA YA KUNGÁTA KALAMU... THEN JAMAA HUYO NA KULA MAKAMASI YAKO YENYE KIFUA KIKUU ARRRGGHHH! ACHENI UCHAFU.
Comment by Mamy Shaluathu on March 16, 2013 at 2:11pm Kaazi kweli kweli.
Comment by Mohamed Sleyim on March 16, 2013 at 1:34pm Ukweli ni kwamba huyu njemba hana pa kutokea kuhusu video hiyo.Hata ukiipeleka lab za majuu bado ni genuine,hana pa kukwepea.
Comment by Monica on March 15, 2013 at 7:52pm
Comment by Joel on March 15, 2013 at 5:18pm Kitaeleweka tu. Hizi ni changamoto za mapinduzi ya demokrasia ya kweli. Watu wasipokata tamaa kitaeleweka tu.
Comment by DORAH FREDY on March 15, 2013 at 4:22pm Makubwwaaaa
Comment by julius manning on March 15, 2013 at 1:56pm Kwa tekinolojia iliyopo sasa ambayo mtu anaweza kuchoa picha halafu akaijaza maneno na matendo , kazi ambayo hata mimi nina programu hiyo katika komputa yamgu inakuwa vigumu sana kuamini . Kwani unaweza kufuta maneno yoyote katika mkanda wowote na kujaza uyatakayo pia vitendo. Lakini ngoja tuache polis wafanye kazi yao kama watashindwa si kuna polis wa martekani huko zanzibar ,kwao hii ni kazi rahisi kabisa.
Comment by Tatu Majaliwa on March 15, 2013 at 12:21pm kwa hiyo tumuamini nani?
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
LJH_3 |
| 5 |
Tatu Majaliwa |
| 6 |
hope |
| 7 |
mayalilwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Matilanga Lukingita |
| 10 |
tina babi |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
© 2013 Created by Global Publishers.





You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers