Gladness Mallya, Dar es Salaam
YAANI we acha tu! Sherehe ya harusi ya msanii mkongwe wa filamu Bongo, William Mtitu imetia fora kutokana na matukio mbalimbali kwenye hafla hiyo, Risasi Mchanganyiko linashuka kifua mbele.
Mtitu alifunga ndoa na mkewe Yovina Swai, Jumamosi iliyopita katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph, Posta jijini Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyochukua nafasi katika Ukumbi wa Urafiki, Ubungo, Dar.
WAONESHA TOFAUTI
Bwana na bibi harusi, badala ya kuingia na muziki wa taratibu kwa pamoja, waliingia huku wakikimbia, kila mmoja na njia yake halafu  wakaanza kulisakata sebene jambo lililoamsha shangwe.
AUNT, WOLPER AIBU TUPU
Masistaduu wanaotesa kwenye ulingo wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na Aunt Ezekiel ndiyo walioongoza kwa mavazi yaliyotia aibu ukumbini.
Wolper alivaa gauni zuri lakini aliharibu kwa kuacha mwili wake wazi kuanzia juu kidogo ya kiuno hadi mabegani kwa kufunika na kijitambaa chepesi cha chekecheke (angalia picha ukusara wa nyuma).
Kwa upande wake Aunt alivaa kigauni kifupi ambapo alilazimika kukaa kwa shida huku akijitahidi kuficha ‘maeneo yake nyeti’ yasionekane, maana kila kitu kilibaki nje huku mabega yake nayo yakiwa wazi.
Mastaa wengine waliovalia magauni yenye mipasuo mikubwa hadi kufikia mapajani ni pamoja na Sabrina Rupia ‘Cathy’, Jenifer Kyaka ‘Odama’, Salama Salmin ‘Sandra’ na Shamsa Ford.
SAJUKI AACHA HISTORIA
Mwigizaji Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ndiye aliyepewa jukumu la kutoa nasaha kwa maharusi, lakini katika hali isiyotarajiwa na wengi, alipita mbele akiwa ameshika kipaza sauti kilichokuwa kikitoa maneno ya kunadi sumu za kuulia wadudu.
“Sumu  ya panya, mende, kunguni, viroboto...” jambo lililowachekesha sana wageni waalikwa.
DOSARI KIDOGO
Aidha kulitokea dosari kadhaa ukumbini humo; mosi, kutokana na udogo wa ukumbi na idadi kubwa ya watu, baadhi ya watu walikosa sehemu za kukaa hivyo kulazimika kusimama wakati wote wa sherehe hiyo huku wengine wakinong’ona kwamba vinywaji (vilevi) ni vichache na vinatolewa kwa kujibana.
“Kamati haikujipanga vizuri...sasa kwa nini walichukua ukumbi mdogo wakati wanajua wageni wao ni wengi hivi? Ona watu walivyosimama! Halafu vinywaji pia vinatolewa kiubabaishaji sana,” alisikika akisema mtu mmoja aliyekuwa jirani na paparazi wetu.

Views: 8810

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by steven emmanuel on September 12, 2012 at 1:55pm

furaha iliyoje kumuona ndugu yetu sajuki anaweza kujichanganya na jamii akiwa na afya tele!!mungu akulinde na akupe afya tele

Comment by rosetarimo86 on September 12, 2012 at 1:29pm

HARUSI YA MILION  25 HALAFU VINYWAJI HAKUNA TENA UKUMBI KIDUCHU HELA ZOOOOOOOOOTE ZIMEISHIA WAPI?AU MLIKUA MNATAFUTA SIFA?

Comment by David Wagwene on September 12, 2012 at 1:01pm

hiyo harusi si ilitangazwa bajeti yake ni 25million inakuwaje wanachukua ukumbi kama kasha la kiberiti na vinywaji vya wakubwa havitoshelezi???????????????

Comment by mayalilwa on September 12, 2012 at 12:11pm

nyie makahaba, nguo fupi mnavaa wenyewe mkitaka kukaa mnakaa kwa shida, ziachieni tu tuzione jinsi zilivyotepeta kwa kusuguliwa hizo naniii....... zenu.

Comment by LEILA BHANJI on September 12, 2012 at 11:54am

honereni sana wapendwa wangu mungu aibariki ndoa yenu na muishi kwa amani na furaha, kikubwa mheshimiane na muwe wakweli. best of love.

Comment by Focus Kunambi on September 12, 2012 at 11:35am

@ FURAHA TAUSI, KUMBE WEWE NI MCHAGA?? POA, LAKINI HII HARUSI TUIPE SIKU NGAPI KABLA HAIJASARAMBATIKA????

Comment by julius manning on September 12, 2012 at 11:33am
mmezoea vya bwete hapo mlikoma ubishooo
Comment by Papaa on September 12, 2012 at 10:20am

Hizo nguo fupi ni biashara ya ukahaba, wanasema ukitaka kahaba nenda bongo movie. Biashara matangazo bwana!!

Comment by FURAHA TAUSI on September 12, 2012 at 9:47am

harusi ikishakosa bia kwa sisi wachaga huwa hatuoni kama imependeza ........

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }