PADR AMLAWITI MFANYAKAZI WA NDANI WA PAROKIA..‏

Na Mwandishi wetu,Moshi.
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro linamsaka Padri Stanslaus Sala wa parokia ya Mtakatifu Theresa Lego Muro,jimbo la Moshi katika kata ya Kilema Kusini kwa tuhuma ya kumlawiti mfanyakazi wa kiume wa parokia hiyo mwenye umri wa miaka 14 (Jina limehifadhiwa).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanaro Lucas Ng’hobko aliithibitisha kupoea kwa taarifa hiyo na kwamba ameagiza padri huyo akamatwe.

“Nimepokea taarifa hiyo jana kutoka kwa wasaidizi wangu na tayari tunafanyia kazi ,anatafutwa kwanza huyu mtuhumiwa wakati upelelezi uiendelea ili kuthibitisha endapo ni kweli amefanya kitendo hicho na ikithibitika tutampelkea mahakamani”alisema Ng’hoboko.


Alisema taarifa za tukio hilo zilifikishwa kituoni Oktoba 31 mwaka huu kufungua jalada ambalo lilipewa namba MS/RB/14614/2010 na kupewa fomu namba 3 (PF 3) kwa ajili ya matibabu ya kijana huyo ambaye alitibiwa hospitali ya mkoa ya Mawenzi.


“Walifika kituoni kufungua jalada na kupatiwa PF 3 kwa ajili ya matibabu,lakini sisi bado hatujaiona inawezekana baada ya kupata matibabu wakaondoka nayo ,tumekwisha sikiliza upande mmoja lakini pia tunahitaji kusikia na upande wa pili”alisema Ng’hoboko.


Awali akizungumza na Tz daima jana mzazi wa kiume wa mtoto huyo,Amati Lyamuya aliyekuwa, ameambatana na wananchi zaidi ya 10 alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 30 mwaka huu,majira ya saa 2 usiku.


Alisema taarifa za mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho zilitolewa na mlinzi baada ya kijana huyo kuonekana kukereka na kitendo hicho kilichofanywa na kiongozi mkubwa kama huyo wa dini.

“Hatukuwa na taarifa yoyote juu ya taarifa ya vitendo vinavyofanywa na huyu Padri ,mlinzi wa parokia ambaye ni mmasai ndiye aliyenda kuwaeleza wazee wa kanisa ambao na wao walikuja kuwaeleza wanakijiji, tukaamua kuandamana”alisema Lyamuya.

Akisimulia tukio hilo ,kijana huyo alisema Padri huyo alimchukua baada ya kuhitimu darasa la saba kwa ajili ya kufanya kazi za kulisha mifugo kwenye Parokia hiyo huku akisubiri matokeo yake.

Alisema siku ya tukio,Padri alimuita mlinzi na kumwagiza akamuite kijana huyo kwenye chumba chake,ambapo baada ya kufika alieleza kuwa anastahili kupewa adhabu na kwamba ataenda kuadhibiwa eneo la mbali na parokia hiyo.

Bila kujua kosa lake kijana huyo alisema waliondoka na alimueleza kuwa wanakwenda eneo la Seminari ya Karumari lakini walipofika eneo la Kisanja ambako kuna msitu ,padri huyo alimtaka kijana huyo ashuke kwenye gari na kumfuata kwa upande wake ambapo alifunga mlango mmoja na kumuegemeza kwenye mlango wa
dereva.

“Baada ya kufika hapo msituni alisimamisha gari akaniambia nishuke na kwenda kwenye mlango wa upande wake ili anipe maelekezo kutoka kwa baba yangu,niliamini na kumfuata’alisema kijana huyo .

Nilipofika alinikandamiza kwenye mlango wa dereva na kunitoa kaptula na nguo ya ndani na kisha kuanza kunilawiti nilijaribi kujiokoa lakini sikufanikiwa ”aliongeza kijana huyo.

Alidai baada ya kumaliza alimwambia apande kwenye gari na kurudi parokiani ambako alienda moja kwa moja chumbani kwake huku akilia kwa uchungu kutokana na kitendo kile.

“Baaada ya kufika chumbani kwangu majira ya saa 5 na 6 Padri alirudi tena kugonga mlango lakini sikufungua’alisema kijana huyo.Alidai kesho yake majira ya saa 2 asubuhi padri huyo alimfuata na kumpa mche mmoja wa sabuni na rozali na kumtaka asiseme popote jambo hilo huku akimuahidi zawadi nyingi zaidi.

Zaidi ya wananchi 10 wakiwa wameandamana na mtoto huyo walifika
kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kufungua jalada lenye
namba MS/RB/14614/2010 na kupewa fomu namba 3 (PF3) ya matibabu kwenye hospitali ya mkoa ya Mawenzi.

Kwa upande wake afisa Mtendaji wa kata,Adamu Mbuya,alisema aliletewa taarifa hizo wakati akiwa ofisini kwake na mwenyekiti wa kijiji,ambapo walimpeleka
hospitalini na kuonekana kuwa amelawitiwa na kujeruhiwa vibaya.

Alisema baada ya kuta taarifa kituo cha polisi walitakiwa kwenda kumkamata Padri huyo lakini zoezi hilo lilishindikana kutokana na polisi kuwa katika zoezi la uchaguzi ,ambapo polisi waliwaambia jalada la kesi hiyo limepelekwa kituo kidogo cha Himo.

Hata hivyo Mbuya alisema jana wakiwa na askari polisi wawili walienda kwenye parokia hiyo na mkuu wa kituo lakini hawakufanikiwa kumpata padri huyo.

Views: 1664

Tags: MLAWITI, PADRI

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by chege on November 18, 2010 at 4:56pm
hawadhalilishi, ila labda kuna mstari wameusoma unaoruhusu kulawit,
mmmmmmmmmhhhhh terrible
Comment by Agnes Francis on November 18, 2010 at 3:37pm
mapadri sasa hivi kazi kudhalilisha kanisa katoliki
Comment by kaka on November 14, 2010 at 2:30pm
upadri ulimshinda dk slaaa kwa mambo kama haya
Comment by abra mohamed on November 13, 2010 at 7:18pm
b nn
Comment by ashuraismailmsemo on November 11, 2010 at 6:26pm
hivi hizi kesi za ubakaji zitaisha lini maana mpaka padri wanabaka kweli dunia imekwisha turudi kwa muumba na tukeshe tukiomba ili jinamizi la ubakaji liondoke maana inatia aibu kwa mapadri namashehe kubaka.
Comment by Mary Stephen Makonda on November 10, 2010 at 4:51pm
du jamani inasikitisha mbona ukristo tnauzalisha jamajiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Comment by Edson Kamugisha on November 10, 2010 at 11:27am
me nafikiri mapadri hawalazimiswi kujiunga na wito huo kwani anapoingia anaamua mwenyewe na kuna sheria inayowaongoza sioni kama kuoa ni solution kama mtu anaona huo si wito wake anaweza kujitoa kuliko kuendelea kulidhalilisha kanisa katoliki na viongozi wao.kila mahali kuna mfumo wake hata nyumba ina sheria zake na kila mtu anayeingia katika nyumba hana budi kutii sheria walizojiwekea wazazi wa nyumba.kikubwa kama uzalendo unawashinda ni kuachia ngazi.wakati wanaapa waliahidi kutekeleza kila linalotakiwa bila kwenda kinyume na utaratibu wa kanisa kwa hiyo wawe waadilifu.
Comment by Mr B on November 10, 2010 at 11:09am
Aibu kwa mtu yoyote anayefanya hivo,.,uogozi uko wapi,.,???
Comment by Agatha Mwasimba on November 10, 2010 at 10:11am
Sheria ichukue Mkondo wake
Comment by JOHN KISAKA on November 9, 2010 at 5:53pm
i cant coment on this because this father is like e dog
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

misu babu posted a status
2 minutes ago
aslam uddin posted a status
2 minutes ago
aslam uddin posted a status
2 minutes ago
misu babu posted a status
3 minutes ago
Shakil Hasan posted a status
3 minutes ago
misu babu posted a status
4 minutes ago
mdsohel173 posted a status
4 minutes ago
misu babu posted a status
5 minutes ago
Profile IconGlobal Publishers via Facebook
Facebook5 minutes ago · Reply
mdsohel173 posted a status
5 minutes ago
misu babu posted a status
5 minutes ago
aslam uddin posted a status
7 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }