Baadhi ya wagonjwa wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
MGOMO wa madaktari unaoendelea nchini tangu Jumatatu ya wiki iliyopita, inasemekana umesababisha vifo vya wagonjwa wanaokadiriwa kufikia 201.
Uchunguzi uliofanywa na timu ya Uwazi tangu mgomo huo ulipoanza, umegundua kwamba kiasi hicho cha wagonjwa waliokufa ni katika mikoa inayokabiliwa na tatizo hilo la madaktari kugoma.
Waandishi wetu Dar es Salaam, walitembelea wodi kadhaa na vyumba vya kuhifadhia maiti vya Hospitali za Temeke, Amana, Mwananyamala na Muhimbili kujionea athari za mgomo huo, huku wa mikoani nao walifanya hivyo.
MUHIMBILI
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, umebaini kuwa wagonjwa wengi wameathiriwa na mgomo huo hali iliyowafanya wajazane wodini bila kupata tiba.
Aidha, timu yetu ilishuhudia wagonjwa wengi wakiwa wamelala chini kwenye korido huku wakiugulia maumivu kwa kukosa huduma ya madaktari.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita mmoja wa wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Samson Maandizi, aliyelazwa Wodi ya Sewahaji alisema tangu alipofika hospitalini hapo kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali ya gari, hajawahi kupata matibabu.
Kufuatia hali tete ya kimatibabu iliyosababishwa na mgomo huo, baadhi ya wananchi wamelazimika kuwahamisha wagonjwa wao na kuwapeleka katika hospitali binafsi.
Hata hivyo, mwananchi mwingine, Hamisi Juma alipohojiwa na gazeti hili hospitalini hapo alisema: “Kutokana na kutokuwa na fedha nimeamua kumhamisha mama yangu na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji Mbagala.”
Kwa upande wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo, mhudumu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema kwamba tangu mgomo huo uanze idadi ya waliokufa mpaka juzi (Jumapili) wanaweza kufikia 57.
MWANANYAMALA
Kwa upande wa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mwananyamala, mmoja wa wahudumu alisema kwamba idadi ya waliokufa kwa kipindi hicho wanaweza kufikia 20.
AMANA
Katika Hospitali ya Amana mhudumu wa chumba cha maiti amesema tangu mgomo huo ulipoanza, watu waliofariki wanaweza kufikia 15.
TEMEKE
Nayo Hospitali ya Temeke hali ni tete kwani inadaiwa nako wagonjwa 19 wamefariki dunia kipindi cha mgomo, kwa mujibu wa mtumishi mmoja wa hospitali hiyo.
BUGANDO MWANZA
Katika Hospitali ya Bugando Mwanza, mmoja wa wahudumu wa chumba cha maiti alimwambia mwandishi wetu mjini humo kwamba kipindi hiki cha mgomo, wagonjwa waliofariki wanaweza kufikia 25.
MBEYA
Mwandishi wetu wa Mbeya, Gordon Kalulunga, anaripoti kuwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoani humo wagonjwa wanaofikia 22 walipoteza maisha na wengine walitoroshwa na ndugu zao wakiwa na dripu baada ya kuona hali zao ni mbaya.
DODOMA
Mwandishi wetu Dodoma anaripoti kuwa mgomo huo umesababidha adha kubwa kwa wagonjwa na inakadiriwa watu tisa wamefariki dunia huku wengi wakirudishwa majumbani kwao.
MOROGORO
Mwandishi wetu, Dunstan Shekidele anaripoti:
Kwa mujibu wa mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro aliyeomba jina lake lihifadhiwe, watu wanaokadiriwa 14 wamefariki dunia tangu mgomo huo ulipoanza.
“Kuna baadhi ya ndugu wamewaondoa wangonjwa wao wakiwa na dripu, kwa kweli hali ni mbaya, tumeambiwa wengine wanafia majumbani,” alisema mhudumu huyo.
KIGOMA, IRINGA NA TANGA
Waandishi wetu katika mikoa hiyo wameripoti vifo idadi yake katika mabano kama ifuatavyo;
Kigoma (nane), Bombo mkoani Tanga (nane) na Iringa (saba).
Hata hivyo, Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Pinda ilikuwa akutane na madaktari Jumapili iliyopita kuzungumzia mgogoro huo lakini ikashindikana kwani Mwenyekiti wa Madaktari, Ulimboka Stephen aliliambia gazeti hili kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ilichelewesha barua ya mwaliko.
Madaktari hao wameitisha mgomo wakidai kuongezewa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu hatarishi , nyumba na usafiri wa kwenda na kurudi kazini.
Comment
Comment by samora rajab albert on February 1, 2012 at 7:55pm MH HATARI, INASIKITISHA KWA KWELI
Comment by mohammed on February 1, 2012 at 9:02am HAKIKA NASIKITISHWA SANA NA KIONGOZI WETU MHESHIMWA RAISI LEO WATANZANIA WANAPOTEZA MAISHA SABABU YA NYONGEZA YA HAKI KWA MADOKTA.
PIA NASIKITIKA SANA KWA MADOKTA KUGOMA KUTIBU WAGONJWA WAKATI PESA HAIWEZI KUNUNUA ROHO YA BINADAMU.
TATU NASIKITI KWETU SISI WANANCHI KITU KAMA HIKI NI MUHIMU KUKITAFUTIA SULUHU.
JAMANI WATANZANIA TUNAELEKEA WAPI WATU 201 WAMEPOTEZA MAISHA NA SERIKALI INGALI INAANGALIA.
TUMUOMBA MHESHIMIWA RAISI AKUMBUKE WAKATI ANAAPA KIAPO MBELE YA MUNGU YA KUWALINDA WATANZANIA NI JUKUMU KUBWA TOKA DUNIANI HADI AKHERA, HAKIKA NDUGU RAISI UNAYO MTIHANI MKUBWA SANA MBELE YA MUNGU.
UNAPOKUBALI MADARAKA NI JAMBO ZITO SANA MBELE YA MUNGU NA SIKU HIYO JAMANI HAIKO MBALI LEO UMRI WA MIAKA 70 UTAFIKIRI MIAKA KUMI KWA JINSI SIKU ZINAVYOKWENDA MBIO.
MHESHIMIWA RAISI NA ALIYEKARIBU NA MHESHIMIWA NAOMBA AFANYE KILA NJIA KILIMALIZA HILI TATIZO SIYO KISIASA BALI KIBINADAMU YARABI LAALAMINI.
PIA NAWAOMBA MADOKTA REJEENI KWA MUNGU NA KUWATIBU WATU KUMBUKENI ROHO ZILIPOTEA MTAULIZWA SIKU YA HESABU.
HAKIKA NINGALIKUWA NIKO TANZANIA NINGALIENDESHA HARAMBE YA KUSAIDIA NDUGU ZETU WAGONJWA, INAUMA SANA KWA VIFO KUSABABISHWA NA VIONGOZI WA SERIKALI WALIOPEWA DHAMANI YA NCHI NA MADOKTA WALIOPEWA DHAAMANA YA KUTIBU.
YARABI MWENYEZI MUNGU TUPE IMANI YA DUNIA NA AKHERA NA TUJUWE KUWA IKO SIKU LAZIMA TUTAONDOKA TENA BILA HATA NGUO HATA PETE KIDOLENI ITATOLEWA.
JAMANI TUFANYE HAKI KAMA TUNAVYOPENDA NAFSI ZETU.
SAMAHANI SANA KWA YOYE NILIYOELEZA NI MIMI NDUGU YENU MOHAMMED NASSER - TOKA DUBA
Comment by Matilanga Lukingita on February 1, 2012 at 2:34am Ndiyo Tanzania hii bana. Mzee anakula mpunga Davos wapiga kura wake wanateketea bongo. Balaa sana hii
Comment by Frank Fungamenza on February 1, 2012 at 1:59am Nadhani katika maisha ya kawaida ukinunua mfano kiatu,kikiaza kukubana njia pekee ni kukiacha sababu kitaendelea kukubanaaaa,badae unapata michubuko miguuni na kuhisi maumivu makari.
Hiki ndio chama chetu,kinatubana lakini hatutaki kubadili kingine!kiatu toka 1961 mpaka leo?...naamini tukibadili hiki kiatu amacho kinatuchubua kila siku,na tunalalamika pasipo mabadiliko,mambo yataenda sawia!...poleni wagonjwa mm nawaombea mpone,lakini madaktari endeleeni kugoma mpaka kieleweke!! jamii ijue uongozi uliopo madarakani ndio unaohusika kwa hili.na kama wameshindwa kutatua hili tatizo,basi wananchi tuelimike tutafute viongozi wanaotufaa kwa matatizo yetu.Wao wakijikwaa tu milangoni kwao ukucha ukatoka haooo India kupata matibabu,sisi je?..mm sipendi unyanyasaji eti kisa ww kiongozi!...unaongoza nini sasa kama wananchi wanakufa haushituki?...kule bungeni watu wanalala eighty-eighty bora hata wangekuwa wanalala fo fo fo,lakini wakifumbua tu macho,fungu hilooo!!...kwanini msiwafanyie hivo na madaktari ambao ni nguzo ya uhai wa wananchi wanaotuchagua mpaka mnaweza kwenda India?...si mlikuwa mnatembelea baiskeli nyie kule kwenu Igombavanu?...uchaguzi utafika tu!!
Comment by Sina Makosa on January 31, 2012 at 9:58pm Waziri wa afya peleka woote jela weka madaktari wapya na mabingwa chukua India kwa mshahara poa tuu tena madakatari wawili wa India sawa na mshahara daktari mmoja wa Bongo
Comment by Sina Makosa on January 31, 2012 at 9:54pm Nyie madaktari hamna akili mmesoma bure badala ya kutumia siasa mnagoma kazi kama kuna jamaa zenu mtawatibu mcdanganye wa2 wanafanya mgoma kwa siku masaa fulani baada ya wiki hamna kutatuliwa tatizo mnaongeza muda mnawapa tena wiki mkimaliza mnatoa onyo lingine kwa kuwapa muda tena kwa kuangalia tatizo ili wajiandar kulitatua tatizo
Comment by Ukweli100 on January 31, 2012 at 8:07pm jamani jamani! viongozi wetu hebu mwogopeni mungu na hizo roho za uwuaji!hawa madaktari wana sababu za msingi kugoma, maisha magumu, mchango wao ni mkubwa na muhimu lakn hawathamniiw, mf mbunge anaye sinzia anakunja at least 200k kwa siku na bado anafisadi na huyu anaye kesha kuhakikisha wa-tz wanarudia afya ananyanyasika wa 10k, kwa kweli serikali kuweni na huruma basi hata kidgo kama hamkujaaliwa nyingi
Nyinyi madaktari mnatuonea tu sisi wananchi ambao tunawategemea nyinyi kwa matibabu.. viongozi wote wanatibiwa India hata wakiumwa mafua .. mnafikiri watasikiliza malalamiko yenu? chondeni madaktari.. rudini hospitalini na kututibia ndugu zenu.. tunaoumia ni sisi watu wa huku chini, , hao viongozi wanapanda ndege na familia zao kwa matibabu safi huko India na sehemu nyingine wanazozijua wao tena kwa pesa za taifa.
Comment by meggie impostra on January 31, 2012 at 6:21pm inatisha jmniiii mhmmmm
Comment by julius manning on January 31, 2012 at 6:19pm kwa kuwa wao wanataibiwa India na jamaa zao ndo maana wanakejeli madaktari badala ya kujitahidi kuelewana nao,ngoja tuishe si ndivyo wanavyotaka
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
LJH_3 |
| 4 |
hope |
| 5 |
julius manning |
| 6 |
mayalilwa |
| 7 |
Tatu Majaliwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Mishy chunga |
| 10 |
shabani abdallah nguluko |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
© 2013 Created by Global Publishers.




You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers