All News Posts Tagged 'saikolojia11' (224)

KWA NINI UWE NA ROHO YA KWA NINI MWENZAKO ANAPOFANIKIWA?-2

NAENDELEA na sehemu ya pili na ya mwisho ya mada hii niliyoianza wiki iliyopita. Niwashukuru wale walionipigia simu na kunipa changamoto ambazo naamini ndizo zinazoweza kuifanya safu hii iwe bora zaidi.

Ndugu zangu, nazungumzia tabia ya baadhi ya watu hasa Watanzania wenzangu kuwa na roho ya kwa nini dhidi ya wenzao waliofanikiwa.

Hii ni tabia isiyofaa ambayo imekuwa ikishamiri sana kwenye jamii yetu, kitu ambacho ni kibaya na kinaweza kurudisha nyuma maendeleo ya…

Added by GLOBAL on May 17, 2013 at 8:30am — No Comments

JINSI YA KUISHINDA HOFU NA NGUVU YA UCHAWI

NAANDIKA mada hii baada ya kuona na kusikia kesi nyingi juu ya watu kuishi maisha yaliyojaa hofu ya kudhurika kwa visasi na vijicho vya wabaya wao.

Hakuna ubishi katika mtazamo wa dunia kwamba kuna maisha chanya na hasi, ambayo yanamzunguka mwanadamu katika safari yake ya kuishi. Lakini ugumu anaoupata mwanadamu na pengine ndiyo ambao nataka kuuzungumzia leo ni jinsi gani anaweza kuishi ndani ya mambo mema na mabaya.

Kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu, nimeona…

Added by GLOBAL on May 16, 2013 at 9:30am — No Comments

KWA NINI UWE NA ROHO YA KWA NINI MWENZAKO ANAPOFANIKIWA?

KAMA wewe ni mfuatiliaji wa safu hii utakubaliana nami kuwa mara kadhaa nimekuwa nikizungumzia mafanikio. Msisitizo wangu katika hilo ni kwamba kila mmoja wetu anayo nafasi ya kufanikiwa endapo ataamua na hata kwenye makala ya wiki iliyopita utakumbuka sikuwa mbali sana na hiki nitakachokizungumza leo.…

Added by GLOBAL on May 10, 2013 at 8:00am — 1 Comment

WIVU KWA WALIOFANIKIWA UTAKUFANYA NAWE UFANIKIWE!

Stori:Amrani Kaima

Neno wivu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, limeelezewa kama hali ama tabia ya mtu kusononeka au kukasirika muda amuonapo mpenzi au rafiki yake ana uhusiano wa mapenzi na mtu mwingine.

Kamusi hiyo pia imeeleza kuwa neno hilo hilo wakati…

Added by GLOBAL on April 26, 2013 at 12:41pm — 1 Comment

FAHAMU JINSI YA KUTUMIA MAJI KAMA TIBA - 2

Hii ni sehemu ya pili na ya mwisho kuhusu unywaji wa maji kama tiba mbadala ya maradhi mbalimbali.  Tafadhali endelea kusoma ili  kujua namna ya kutumia maji kama tiba.  



PILI: Kutokana na shinikizo hilo la maji la…

Added by GLOBAL on April 23, 2013 at 11:57am — 1 Comment

TUKIISHI KIBUBUSA MAFANIKIO LAZIMA YATUPITIE PEMBENI!-2

Awali ya yote tumshukuru Mungu kwa mema ambayo amekuwa akitutendea katika kila siku ya maisha yetu.

Kikubwa tumshukuru kwa kutufanya kuwa miongoni mwa wale wanaoendelea kupumua kwani wapo ambao muda huu wako hoi mahospitalini huku wengine wakiwa tayari wametangulia mbele za haki.

Ndugu zangu, wiki iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia umuhimu wa kila mmoja wetu kuishi kwa malengo na kufanya kila linalowezekana kuwa na mafanikio katika maisha yake.

Kipindi hiki si cha…

Added by GLOBAL on April 20, 2013 at 3:47pm — No Comments

MAWAZO YA MASKINI NA TAJIRI YANAVYOTOFAUTIANA-3

KUFANIKIWA maishani siyo jambo linalotokea kama bahati.  Katika njia ya kuelekea kwenye mafanikio, kuna vikwazo vingi sana ambavyo mtu anaweza kukumbana navyo.  Unapokumbana na vikwazo vingi haina maana kuwa una bahati mbaya au umerogwa.

Baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuyakuza matatizo hata kama ni madogo kiasi gani. Unakuta mtu akikumbana na kikwazo kidogo anakuwa mwepesi wa kulaumu, atalalamika akiomba msaada kwa kila mtu.  Ukiona mtu yuko hivi basi ujue ana…

Added by GLOBAL on April 11, 2013 at 8:25am — 2 Comments

MAWAZO YA MASKINI NA TAJIRI YANAVYOTOFAUTIANA-2

WATU karibu wote ulimwenguni wanatamani kuwa matajiri na kumiliki mali. Kila mmoja anapenda siku moja ayamudu maisha yake kwa kila kitu. Awe na nyumba nzuri, gari zuri, familia bora na maisha bora kwa ujumla. Lakini ni wachache sana kati yetu tunathubutu kujitoa kwa moyo mmoja kupigania  kile tunachokitaka.

Utajiri sio kituo au mahali ambapo utajikuta tu ukiwa tajiri. Lazima ufahamu unatakiwa kufanya nini ili ufike pale unapotaka. Lazima ujibidiishe usiku na mchana kwa…

Added by GLOBAL on April 4, 2013 at 9:00am — 1 Comment

UNAPOPATA FEDHA, ‘USIZITUMBUE’ KANA KWAMBA KESHO HAIPO!

Leo nataka kuzungumzia tabia ya baadhi ya watu kutumia fedha wanazozipata kwa fujo kana kwamba wameambiwa kuwa kesho wanakufa. Hakuna asiyefahamu umuhimu wa pesa, na kutokana na hilo, wengi wamekuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha wanazipata.…

Added by GLOBAL on March 29, 2013 at 9:13am — 3 Comments

HATARI! ‘MAHAUSIGELI’ WENGI WAMEPITIA UKAHABA-2

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

“Kusema ukweli nawalea vizuri, ila mtoto akiniletea ujinga nampa mbata (anampiga). Unajua tatizo ni kwamba, kuna wakati hawa watoto wa matajiri siyo. Unampa msosi ale alale ili na wewe uweze kwenda kwenye mambo yako, akishakula halali wala nini? Ukimlazimisha anajifanya…

Added by GLOBAL on March 28, 2013 at 3:54pm — 5 Comments

UKE WENZA AU MUMEO KUWA NA VIMADA KWA SIRI KIPI BORA?-3

WIKI hii nitaimalizia mada hii ili wiki ijayo nigeukie kitu kingine. Niwashukuru tu wale ambao wamekuwa wakinitumia ujumbe na wengine kunipigia simu kunipongeza kwa kile ambacho nakiandika kupitia safu hii.

Tunachotakiwa kujua ni kwamba, nyumba ndogo zipo tena hizi ndizo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa mapenzi baina ya wale walio katika ndoa na wakati mwingine kuvunja ndoa.

Nyumba ndogo zimekuwa zikijitahidi kutoa huduma nzito kwa waume za watu hadi kufikia…

Added by GLOBAL on March 22, 2013 at 8:30am — No Comments

JINSI YA KUPATANA NA MTU ULIYEKOSANA NAYE

KWA kuwa migogoro ni moja kati ya mambo yanayotokea katika safari ya maisha si vibaya tukajifunza namna ya kuikabili. Kwa bahati mbaya tafiti zinaonyesha kuwa kiwango cha migogoro ni kikubwa miongoni mwa jamii ukilinganisha na watu wenye ufahamu wa kuitatua.

Watu wamekuwa wakifanyiana ukatili, nchi zikipigana vita kwa sababu ya migogoro mbalimbali ambayo ingepata wajuzi…

Added by GLOBAL on March 21, 2013 at 8:00am — 6 Comments

UKE WENZA AU MUMEO KUWA NA VIMADA KWA SIRI KIPI BORA?-2

NAENDELEA na makala haya ambayo niliyaanza wiki iliyopita. Lengo ni kuzungumzia uke wenza na utitiri wa vimada huko mtaani tunakoishi.

Suala kubwa ni kwamba, hakuna raha katika kuchangia penzi na wengi wanaamini penzi haliwezi kugawanyika hivyo mwanaume anapoamua kuwa na wake wawili ama zaidi, ajue lazima kati ya hao mmoja atajisikia mnyonge, asiyependwa.

Kwa…

Added by GLOBAL on March 15, 2013 at 9:14am — 5 Comments

Marafiki wanavyoweza kukufanya usifanikiwe

MARA nyingi nimeeleza  katika mafundisho yangu kwamba mawazo yetu yakitupa majibu kwamba vitu tunavyotaka kuvifanya vinawezekana, bila shaka tunaweza kutenda hata kama vitakuwa vigumu kiasi gani kwa sababu mawazo yanayotuongoza hupita vikwazo vya matatizo yetu.

Kwa upande mwingine chochote tunachoamini kuwa hakiwezekani, hatuwezi kuwa na msukumo wa kujaribu kwa vile hofu ya kushindwa huongeza udhaifu wa mwili.  Wanasaikolojia maarufu akiwemo Lakshmi Aiyer wamethibitisha…

Added by GLOBAL on March 14, 2013 at 8:00am — 1 Comment

UKE WENZA AU MUMEO KUWA NA VIMADA KWA SIRI KIPI BORA?

NI wiki nyingine mpenzi msomaji tunakutana tena katika safu hii ambayo lengo lake hasa ni kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayogusa maisha yetu ya kila siku.  

Wiki hii nitazungumzia uke wenza na jinsi unavyowatesa baadhi ya wanawake.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa, wanawake wengi…

Added by GLOBAL on March 8, 2013 at 11:23am — 3 Comments

JINSI YA KUFANYA UNAPOFELI MITIHANI-2

Inaelezwa kuwa kipindi cha kati ya mwezi mmoja na miwili baada ya matokeo kutolewa huwa ni hatari kwa uharibifu wa akili za wanafunzi waliofeli.

Wengi kati ya wanafunzi waliofeli huanza kuharibika kitabia muda mfupi baada ya kupoteza matumaini kutoka katika masomo yao. Uchunguzi unaonyesha vijana wengi huingia vijiweni na kuanza utumiaji wa dawa za…

Added by GLOBAL on March 7, 2013 at 10:00am — 2 Comments

MSEMO WA ‘KUFELI MTIHANI SIYO KUFELI MAISHA’ UNAVYOWAHARIBU VIJANA!-2

NINA kila sababu ya kumshukuru Mungu ambaye amenibariki kuwa mmoja kati ya wale waliobahatika kuiona siku ya leo wakiwa bukheri wa afya.

Ni matumaini yangu kuwa, nawe umzima na uko tayari kusoma sehemu ya pili ya makala haya ambayo niliianza wiki iliyopita.

Lengo hasa la makala haya ni…

Added by GLOBAL on March 1, 2013 at 10:17am — No Comments

JINSI YA KUFANYA UNAPOFELI MITIHANI

LK Johnson Profesa wa zamani kutoka Chuo cha Stanford nchini Uingereza, aliwahi kusema kuwa mwanafunzi anaweza kupasi mtihani wake kabla hata hajaufanya kutokana na kujiamini kwake.

Hata hivyo, hatari inatajwa kuwa kubwa kwa mwanafuzi wa aina hiyo pale linapokuja suala la kufeli mtihani.

Wanafunzi wengi hujiuliza baada ya kushindwa mtihani wafanye nini kukabili changamoto za kimaisha? Idadi kubwa ya wenye maswali haya ni wale wanaotoka katika familia masikini…

Added by GLOBAL on February 28, 2013 at 9:00am — No Comments

MSEMO WA ‘KUFELI MTIHANI SIYO KUFELI MAISHA’ UNAVYOWAHARIBU VIJANA!

MSEMO wa kwamba kufeli mtihani siyo kufeli maisha umekuwa ukitumiwa sana na vijana wengi. Mara ya kwanza kuusikia ilikuwa wakati nasoma kidato cha pili kipindi ambacho tulikuwa tunajiandaa na mtihani wa taifa.

Nilimsikia mwanafunzi mmoja akimuamsha rafiki yake ili waende wakajisomee. Yule kijana alipokurupuka nilimsikia akimweleza yule rafiki yake maneno haya: “Bwanaee!  Mimi siendi kusoma na siogopi kufeli mtihani. Kufeli mtihani siyo kufeli maisha.”

Maneno hayo…

Added by GLOBAL on February 22, 2013 at 10:56am — No Comments

MBINU ZA KUWASHAWISHI WATU WAKUSAIDIE

WATU wengi tunapokuwa kwenye mikwamo huwa tunatamani sana kuona wenzetu wanatusaidia. Yawezekana hata unaposoma makala haya kuna mambo unahisi unahitaji msaada kutoka kwa binadamu wenzako lakini hao unaotarajia wakusaidie inaonekana kama wamekupa kisogo.

Katika kazi yangu ya ushauri wa masuala ya Elimu ya Ufahamu na Nafsi nimekuwa nikikutana na watu wengi wenye matatizo makubwa ambayo kusema kweli yanahitaji msaada wa wasamaria na wakati mwingine hata kutoka kwa bosi…

Added by GLOBAL on February 21, 2013 at 8:31am — No Comments

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE yesterday. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

Latest Activity

Terese Forsyth posted a status
1 hour ago
Tania Montero posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
""
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago
Olga Bliss posted a status
1 hour ago

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service