All News Posts Tagged 'mikasa11' (898)

Kitanzi, Kisu au Bastola - 18

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

“Angalia!” aliongea Madam Flaviana huku akimpatia bahasha ndogo Side aliyeipokea kwa wasiwasi na kuifungua.

“Ndiye, siye?” aliuliza Madam Flaviana akimtazama Side aliyekuwa akizikodolea picha alizozitoa ndani ya bahasha ile.

Tiririka Nayo...

“Vipi?” Madam Flaviana aliuliza tena baada ya kumuona Side akitetemeka kwa hofu kama mtu aliyeona jini.

Picha zilikuwa sawa kabisa na…

Added by GLOBAL on May 23, 2013 at 8:30am — 3 Comments

Lusifa Aliniita Kuzimu-34



MPENZI msomaji, kijana David anaendelea kusimulia kisa kilichomkuta katika maisha yake, wiki iliyopita niliishia pale alipopigwa na kitu kizito kichwani. Je, nini kilitokea? SONGA MBELE MDAU WANGU…

Baada ya kupigwa na kitu hicho, kichwa kikawa kizito, nikaanza kuona maghorofa yote yaliyopo Posta yanazunguka na mwili wote ukaanza kuwaka moto.

Kufuatia maumivu ya moto niliyoyapata nikaanza kupiga kelele huku nikiomba msaada lakini sikupewa.

Wakati nikilia…

Added by GLOBAL on May 23, 2013 at 8:30am — 2 Comments

MAMA YANGU ADUI YANGU - 42

ILIPOISHIA:

“MAMA yako angeniona na kitu hicho angeanguka, ndiyo maana nilitakiwa nikuache na kuondoka haraka. Kama ningeendelea kuwepo kwenu, mama yako angekufa.”

“Ni kwa nini?” niliuliza mkono wangu ukiwa shavuni.

SASA ENDELEA...

“Kwa sababu ya ubaya wake,” alisema.

“Unafikiri kwa nini amekuwa na tabia hiyo?” nilimuuliza swali ambalo nilitakiwa nilijibu mimi mwenyewe.

“Ni roho mbaya na kupenda…

Added by GLOBAL on May 22, 2013 at 9:16am — 6 Comments

Macho ya Bundi-18

“Wewe unaingilia yanakuhusu?... Yanakuhusu? Badala ya kurudi nyumbani kwako, unang’ang’ania katika nyumba za watu na kuziharibu. Umechangia sana kutugombanisha wewe,” nilimjibu.

Mume wangu alikuwa amesimama katikati ya sebule huku akitokwa na jasho jingi usoni kana kwamba alikuwa anafanya mazoezi ya judo. SONGA NAYO...

BADALA ya kusikiliza upuuzi aliokuwa akiusema Pili na mama yake, nilikwenda chumbani kwangu na kumuacha mume wangu akiwa amesimama…

Added by GLOBAL on May 21, 2013 at 9:46am — 5 Comments

Wakala wa Shetani - 27

“Bwana eeeh tuchimbe dawa hapa.”

“Sawa.”

Kusekwa alitulia akijua jamaa wameteremka kwenda kujisaidia haja ndogo, wakati wanaingia kwenye gari ili waondoke, aliteremka haraka na kuliacha gari liende. Sehemu aliyoshuka ilikuwa ngeni kwake. Kulikuwa na vichaka ambavyo hakuwa na uhakika wa usalama wake.

SASA ENDELEA...

baada ya kutoka ndani ya kinywa cha mauti aliamini alikuwa salama, wakati akitafakari afanye…

Added by GLOBAL on May 18, 2013 at 9:59am — 4 Comments

MAMA YANGU ADUI YANGU - 41

ILIPOISHIA:

“Si nilikuuliza nani anataka kukubakiza jina huniambii ikabakia siri yako na familia yako huku ukitaka kunigombanisha na mama yangu.”

“Samahani naomba tutafute sehemu nzuri  tuzungumze vizuri.”

SASA ENDELEA...



“Leo ndiyo unaweza kumsema?” nilimuuliza nikiwa nimemkazia macho.

“Kama mpaka leo hujui tatizo lazima nikueleze huenda likaiokoa ndoa yako ya sasa.”

Kauli ile ilinifanya niwe na…

Added by GLOBAL on May 18, 2013 at 9:30am — 4 Comments

Kitanzi, Kisu au Bastola - 17

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Sonia alikumbuka vyema siku ambayo alimuona Side akitetemeka kwa hofu ya kuua kama alivyomuona siku hiyo. Alikumbuka ambavyo alitamani kuifutilia mbali tarehe na mwezi ule ili isahaulike kabisa kutoka kwenye kalenda. Siku hiyo yeye Sonia, alikuwa ndiye mtu aliyetakiwa kuuawa na Mr. John Chakos.

ENDELEA...

Side aliyeiseti vyema bunduki yake katikati ya paji la uso wa Sonia, hakuweza kufanya chochote…

Added by GLOBAL on May 16, 2013 at 9:30am — 2 Comments

Lusifa Aliniita Kuzimu-33

MPENZI msomaji, kijana David anaendelea kusimulia mkasa uliomkuta katika maisha yake. Wiki iliyopita niliishia pale alipokwenda kwenye hoteli ya nyota tano kwa lengo la kuwaroga matajiri ili wapate maradhi lakini alipofika akagundua kwenye moja ya vyumba kulikuwa na mchungaji ambaye alijua atamharibia mambo yake ndipo akaamua kwenda kumuua. Je, alifanikiwa? Tuwe pamoja…

Lusifa aliponiambia hivyo bila kujua ningepewa masharti gani nilifurahi sana na kumwambia nilikuwa…

Added by GLOBAL on May 16, 2013 at 9:30am — 2 Comments

MAMA YANGU ADUI YANGU - 40

ILIPOISHIA JUMAMOSI:

  Naweza kupata mwanaume mwingine mambo yakawa yaleyale.”

“Nakuhakikishia matatizo yaliyotokea hayatatokea tena.”

“Kivipi?”

“Tatizo lililokuwepo nimeshalimaliza japokuwa ilikuwa kazi nzito.”

“Unaweza kuniambia nani aliyefanya mchezo huu?”

“Wapo wawili, mmoja mke wa huyu mzee na mwingine nina imani naye ameachana na mchezo huu,” mama…

Added by GLOBAL on May 15, 2013 at 8:53am — 6 Comments

Macho ya Bundi-17

ILIPOISHIA:

Pili siku zake za kujifungua zilifika ikawa yupo hospitali kwenye chumba cha kujifungulia, yaani leba. Mimi, mume wangu Chinchi na Mei tulikuwa nje ya chumba hicho huku nikiwa kama nasikia maneno ya Mei, “…Pili ana mimba, akipatwa na matatizo wakati wa kujifungua nitajua ni wewe,”

SONGA NAYO...

Tulikaa nje ya hospitali hiyo kwa saa kadhaa kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani. Mume wangu Chinchi alionekana kuwa…

Added by GLOBAL on May 14, 2013 at 9:00am — 4 Comments

Mama Yangu Adui Yangu - 40

ILIPOISHIA:

“Nikusaidie nini dada? Kama kazi sasa hivi hakuna, nyumba imemalizika. “

“Sina shida hiyo.”

“Una shida gani?”

“Samahani kaka una muda gani hapa?”

SASA ENDELEA...

“UNAMAANISHA kuwepo hapa kivipi?”

“Kikazi.”

“Huu mwezi wa pili, kwani vipi?” mlinzi alionesha kunishangaa.

“Ndiyo maana hunifahamu.”

“Kwani wewe ni…

Added by GLOBAL on May 11, 2013 at 7:58am — 3 Comments

Wakala wa Shetani - 27

Alipopapasa vizuri, aligundua ile ni Toyota Pick Up, akiwa anajiuliza pale ni  wapi, mara umeme uliwaka. Kusekwa alijiona yupo kwenye maegesho ya magari, kabla hajaamua afanye nini aliwasikia watu wakielekea kwenye gari hilo huku wakizungumza.

“Inabidi tuwahi kuondoka muda huu mzigo umefika tangu saa saba.”

“Itakuwa vizuri, Mr Brown alikuwa hana raha kabisa.”

Sauti zile zilimfanya Kusekwa aingie chini ya gari na…

Added by GLOBAL on May 11, 2013 at 7:55am — 2 Comments

Kitanzi, Kisu au Bastola - 16

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Alishinda akimuangalia Salima alivyokuwa akioga na kuvaa nguo zake na hata pale alipokuwa akitembea ndani ya korido za jengo hilo. Nafsi yake ilianza kujaa tamaa ya kufanya mapenzi na msichana huyo.

SONGA NAYO...

Salima kwa upande wake aliamka asubuhi na mapema akiwa na nia ya kumuuliza Madam Flaviana kama mpenzi wake, Dedan alikuwa amepatikana. Akatembea akikatiza korido kadhaa akikielekea chumba…

Added by GLOBAL on May 9, 2013 at 9:30am — 1 Comment

Lusifa Aliniita Kuzimu-32

Mpenzi msomaji, kijana David anaendelea kusimulia mkasa uliomkuta katika maisha yake. Wiki iliyopita niliishia pale alipokwenda kwenye hoteli yenye  hadhi ya nyota tano kwa lengo la kuwaroga matajiri ili wapate maradhi lakini alipofika akagundua kwenye moja ya vyumba kulikuwa na mchungaji ambaye alijua atamharibia mambo yake ndipo akaamua kwenda kumuua. Je, alifanikiwa? Tuwe pamoja…

Nilipoingia mle chumbani kichawi nilimrushia pepo mchafu ili amvuruge akili ndipo…

Added by GLOBAL on May 9, 2013 at 9:30am — 2 Comments

MAMA YANGU ADUI YANGU -39

ILIPOISHIA:

Da’ Suzy ambaye alikuwa amekuja kwa muda Dar baada ya kuhamia Mwanza na mumewe. Alinieleza alivyonikuta siku aliyokuja kunitembelea.

“Mwaija Mungu mkubwa,” alisema huku akiniangalia kwa jicho la siamini.

“Kwa nini?”

“Nilivyokukuta siku ya kwanza na leo hii tunaongea hivi naamini Mungu mkubwa na Mungu yupo pia mama Amina mganga.”

“Kwani…

Added by GLOBAL on May 8, 2013 at 9:00am — 7 Comments

Macho ya Bundi-16

ILE kufungua tu chumba chetu ili tutoke, tulikutana uso kwa uso na Mei akiwa amesimama.

“Wewe mkwe nimesikia kila kitu ulichosema na mkeo kwamba ni vyema mlale chumba kimoja na mwanangu. Utamaduni wa wapi huo? Huyu Salome badala ya kukupa ushauri anachekelea kwenda kumvurugia mwanangu unyumba?”

“Lakini rafiki yangu…”

“Rafiki yako nani? Huoni jinsi unavyomvurugia mwanangu. Siku ya kwanza tu katika ndoa yake unaanza…

Added by GLOBAL on May 7, 2013 at 8:30am — 7 Comments

MAMA YANGU ADUI YANGU -38

ILIPOISHIA:

Kauli ya mama Amina niliiamini kwa asilimia ndogo sana kwa kuamini aliyosema ilikuwa kunipa moyo. Ajabu mwili wangu  ulikuwa mwepesi tofauti na siku za nyuma ambao niliusikia mzito kama nimebebeshwa mzigo kizito hata kuhema kwangu kulikuwa kwa shida lakini baada ya zoezi lile nilihema vizuri.

Nilikaa kwa mama Amina kwa siku kadhaa huku nikiendelea kutimia dawa zake.Alinieleza jini nililotupiwa lilitaka kufanya viungo vyangu…

Added by GLOBAL on May 5, 2013 at 12:53pm — 4 Comments

Wakala wa Shetani - 26

MIAKA SABA BAADAYE

Kusekwa aliendelea kukua, akafikia hatua ya kwenda shule iliyokuwa katika kambi hiyo, akaanza chekechea na kuandaliwa kwenda shule ya msingi. Lakini kabla hajaanza shule ya msingi alitokea Mzungu mmoja aliyekuwa akimiliki machimbo ya dhahabu.

Mzungu huyo aliyejulikana kwa jina la John Brown ‘Mr Brown’ alikuwa na mgodi mkubwa uliokuwa na wachimbaji wengi sana. Kutokana na uwezo wake wa kifedha aliweza kuwasaidia wanakijiji…

Added by GLOBAL on May 4, 2013 at 9:49am — 3 Comments

Kitanzi, Kisu au Bastola - 15

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA

Kiu na njaa kali vilimfanya Dedan adhoofu na kupoteza fahamu kabisa. Akalala kifo kikimnyemelea, ubongo wake ukiimba nyimbo za huzuni huku taswira na jina la msichana mzuri aitwaye Carolina ikififia kichwani mwake.

Songa Nayo...

Usiku huo giza lilikuwa nene kupita kiasi. Watu wengi tayari walisharudi kutoka kwenye mihangaiko ya kila siku na kujifungia majumbani mwao. Hakuna hata mmoja aliyejua kama kuna…

Added by GLOBAL on May 2, 2013 at 9:24am — 2 Comments

MAMA YANGU ADUI YANGU -37

ILIPOISHIA:

Ilikuwa baada ya kupoteza fahamu kwa siku mbili, kilichositisha kuzikwa kwangu ni joto la mwili ambalo wazee walisema wanaweza kunizika nikiwa bado hai.

Baada ya hapo sikuelewa kilichokuwa kikiendelea mpaka niliposhtuka pale nilipopiga chafya mfululizo.

Nilipofumbua macho nilijikuta sehemu ambayo haikuwa ngeni lakini bado sikuwa na uhakika nayo.

Nilipojaribu kunyanyuka nilishindwa,…

Added by GLOBAL on May 1, 2013 at 9:00am — 6 Comments

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service