All News Posts Tagged 'jumatano11' (2,418)

Mwili wa mdogo wa Julio kutua keshokutwa

Na Martha Mboma

MWILI wa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Malindi FC ya Zanzibar na Twiga FC,  Chaku  Mussa Kihwelo ambaye pia ni mdogo wa kocha wa zamani wa Simba na sasa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, unatarajia kutua nchini Ijumaa wiki hii kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).

Marehemu alipatwa na umauti wiki iliyopita nchini Afrika Kusini baada ya kumwagiwa maji ya moto akiwa usingizini na rafiki yake raia wa Zimbabwe baada ya kutokea…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 10:20am — No Comments

Kopunovic awaweka wachezaji wake kitimoto kwa dakika 50

Wilbert Molandi na Martha Mboma

KOCHA Mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic, juzi Jumatatu alitumia dakika 50 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wachezaji wanaounda kikosi hicho katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na  Azam FC katika mechi ya ligi kuu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Kikao hicho kilianza kufanyika majira ya saa 10:30, kikamalizika saa 11:20 jioni kwenye Ufukwe wa Dege…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 10:20am — No Comments

Yondani, Niyonzima watupwa nje Yanga SC

Na Hans Mloli

WACHEZAJI wawili wa kikosi cha kwanza Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na Kelvin Yondani, wameenguliwa kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoendelea kujipanga kwenye mechi ijayo dhidi ya Ndanda FC kutokana na kuwa majeruhi.

Niyonzima na Yondani waliumia kwenye mechi ya wikiendi iliyopita walipoumana na Polisi Moro, katika mchezo uliomalizika kwa Yanga kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0.

Wachezaji hawa hawakuwepo kwenye…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 10:20am — No Comments

MZEE YUSUF: SIKU YA WAPENDANAO INANITAMBUA

Na Omary Mdose

MFALME wa muziki wa Mwambao, Mzee Yusuf amefungukia sikukuu ya wapendanao ambayo hufanyika kila mwaka Februari 14 na kusema kuwa siku hiyo huwa anakumbukwa kupitia wimbo wake wa My Valentine.

Akizungumza na gazeti hili, Mzee Yusuf akiwa na kundi lake la Jahazi linalosumbua na albamu ya Chozi la Mama alisema kuwa, aliamua kuimba wimbo huo ambao utakuwa ni zawadi kila mwaka katika siku kama hiyo ya wapendanao.

“Lengo haswa la…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 10:20am — No Comments

Kagera watumiwa ujumbe wa uchawi, waikimbia Kirumba

Na Nicodemus Jonas

UONGOZI wa Kagera Sugar umeamua kuhamia mkoani Shinyanga na kuachana na Uwanja wa CCM Kirumba kwa kile kilichotajwa kurogwa na wenyeji wa uwanja huo, Toto African, kwa sababu zilizotajwa kuwa waliapa kuhakikisha Kagera haitoki na pointi uwanjani hapo.

Chanzo cha bifu lao ni kwamba Toto wanalipiza kisasi cha Kagera kuwabania misimu miwili iliyopita ambapo iliwafunga katika mchezo wa mwisho, kichapo kilichowashusha daraja Toto…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 10:19am — No Comments

Simba, Mbeya City zavimbishiana

Na Martha Mboma

WAKATI timu za Simba na Mbeya City zikitarajiwa kushuka dimbani leo, Mbeya City imetamba kuwa itahakikisha inaibuka na ushindi ili kuweza kuwa katika nafasi nzuri zaidi huku Simba nao wakiahidi ushindi.

Timu hizo zitavaana katika Uwanja wa Taifa  jijini Dar, ukiwa ni mchezo wa kiporo ambao ulitakiwa uwe umekwishachezwa tayari lakini michuano ya Kombe la Mapinduzi iliweza kuzuia.

Msimu uliopita, timu hizo zilipokutana, mara…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 10:19am — No Comments

JIPATIE NAKALA YAKO YA CHAMPIONI JUMATANO

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 9:55am — No Comments

Coutinho aomba kucheza Taifa Stars

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili,…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 9:54am — No Comments

Wazazi wamwambia Tambwe arudi Burundi

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 9:54am — No Comments

Okwi amwaga chozi akisimulia

Kiungo mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel…

Added by GLOBAL on January 28, 2015 at 9:54am — No Comments

yanga yatinga TFF sakata la Tambwe

Na Khadija Mngwai

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa unasubiria kuona Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), litachukua hatua gani kutokana na kitendo cha mshambuliaji wake Amissi Tambwe kukabwa koo na mchezaji wa Ruvu Shooting.

Tambwe alichezewa rafu kadhaa na beki wa timu hiyo, George Michael, mpaka akachanika mdomoni lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote.Katika mchezo wa Jumamosi kati ya Yanga na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa,…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 10:04am — 1 Comment

Azam FC yaizamisha Kagera, yarejea kileleni

Na Martha Mboma

HATIMAYE mabingwa watetezi, Azam FC, wamerejea kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 3-1, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo huo, Azam ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya pili kupitia kwa mshambuliaji wao Muivory Coast, Kipre Tchetche, baada ya kupata pasi safi kutoka kwa kiungo Mudathir Yahaya.

Mchezo huo ulionekana kuwa na…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 10:04am — 1 Comment

Sserunkuma awatangazia vita mabeki

Na Nicodemus Jonas

BAADA ya kufungua akaunti yake ya mabao kwenye Klabu ya Simba, straika Dan Sserunkuma, ametangaza hali ya hatari kwa timu za ligi kuu kwa kusema kuwa tayari ameondoa ‘gundu’ na Wanasimba wasubiri vitu vyake.

Mganda huyo alianza vibaya ambapo alikuwa akiandamwa na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kucheza chini ya kiwango, lakini kadiri siku zinavyokwenda amekuwa akizidi kuonyesha kiwango cha juu.

Wikiendi iliyopita…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 10:03am — 1 Comment

Kopunovic atawala na Kiswahili mazoezini

Martha Mboma na Sweetbert Lukonge

KATIKA kuhakikisha kile ambacho anafundisha wachezaji wake wanakielewa vyema kocha mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic ameamua kutumia  baadhi ya maneno ya lugha ya Kiswahili katika kuwafundisha wachezaji wake.

Maneno kama cheza, geuka, piga kule yamekuwa yakitumiwa na kocha huyo mazoezini na kuwafanya mashabiki mara kwa mara wafurahie.

Kikosi cha Simba jana kilianza mazoezi rasmi katika Uwanja wa Boko…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 10:03am — 1 Comment

Pluijm apata dawa ya Tambwe, Kpah Sherman

Na Wilbert Molandi

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amesema amepata dawa inayosababisha washambuliaji wake washindwe kufunga mabao kwenye mechi.

Mholanzi huyo aliona upungufu huo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, iliyomalizika Jumanne iliyopita huko visiwani Zanzibar kwa Simba kutwaa taji hilo kwa kuwafunga Mtibwa Sugar.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inaongozwa na Mliberia, Kpah Sherman, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda,…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 10:03am — 3 Comments

JIPATIE NAKALA YAKO YA CHAMPIONI JUMATANO

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 9:43am — No Comments

Milioni ya Yanga yamvuruga Ngassa

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 9:43am — 2 Comments

Baba Manyika amtaka mwanaye

Mlinda mlango wa Simba, Peter…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 9:42am — 1 Comment

Tambwe, beki ‘katili’ ugomvi wao ulianzia Simba

Beki wa Ruvu Shooting, George Michael akimkunja Amissi…

Added by GLOBAL on January 21, 2015 at 9:42am — 1 Comment

Mastaa Simba SC, Yanga wavurugana

Na Nassor Gallu

MASTAA waliowahi kuwika wakiwa na timu kongwe za Simba na Yanga miaka ya nyuma, walizua tafrani Jumapili iliyopita wakati timu zao za sasa, Friends Rangers na Villa Squad, zilipokutana kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar.

Siku ya mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, mastaa walioiongoza Friends walikuwa ni Haruna Moshi ‘Boban’, Yusuph Mgwao, Amir Maftah na Credo Mwaipopo wakati…

Added by GLOBAL on January 14, 2015 at 10:37am — 1 Comment

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha Jan 9. 0 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa Jan 9. 0 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa Jan 6. 0 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka Jan 6. 0 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by maleka sakeha Jan 5. 4 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by maleka sakeha Jan 5. 17 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by lee chong wei Dec 28, 2014. 31 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by damarr on Thursday. 89 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

TOP NEWS WEEK HII

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }