All News Posts Tagged 'hadithi11' (2,311)

THE END OF TORTURE-93

Ule usemi wa wahenga kwamba ukiona giza linazidi kuongezeka ujue mapambazuko yamekaribia unaonekana kutimia kwenye maisha ya msichana mdogo, Amelia. Baada ya kuteseka kwa kipindi kirefu tangu akiwa bado mdogo, hatimaye mapambazuko yanaanza kuonekana kwenye maisha yake.Mateso makali aliyowahi kuyapitia katika maisha yake yote yanabaki kuwa historia.

Alianza kuteseka tangu akiwa na umri mdogo sana ambapo aliwapoteza wazazi wake wote wawili,…

Added by GLOBAL on September 17, 2014 at 8:54am — 5 Comments

THE BLOOD STAINED DRAFT-40

Muungano uliodumu kwa kipindi kirefu kati ya Bara na Pwani, watu kutoka pande hizo zote mbili wakiishi kwa amani na upendo na kushirikiana mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kiserikali, unaingia shubiri na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wasio na hatia.

Ushirikiano mzuri uliokuwepo tangu awali unavunjika, watu kutoka pande hizo mbili wanashambuliana kwa mapanga na silaha nyingine za kienyeji na kusababisha wengi kupoteza maisha…

Added by GLOBAL on September 17, 2014 at 8:51am — 5 Comments

Golden Tears (Machozi ya Dhahabu) - 31

Muigizaji mkubwa na maarufu nchini Tanzania, Goodness anahangaika kwa kipindi kirefu akisaka mtoto. Licha ya kutembea na wanaume wengi akiwa na ndoto ya kupata mtoto, muigizaji huyo anashindwa kutimiza ndoto hiyo kwani kila mwanaume anayekuwa naye, anamtumia na kumuacha.

Baada ya kutembea na mwanamuziki aliyekuwa akitikisa, Golden na kuoana naye, hatimaye Goodness anafanikiwa kupata watoto, ila tatizo ni pale anapoambiwa kwamba watoto hao wameungana. Japokuwa…

Added by GLOBAL on September 17, 2014 at 8:51am — 5 Comments

TRUE LOVE-5

Ebola, ugonjwa hatari usio na tiba wala kinga, unaikumba Liberia, nchi iliyopo Magharibi mwa Bara la Afrika na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wake. Watu wengi wanaambukizwa ugonjwa huo na ndani ya muda mfupi tu, mamia ya wananchi wanapoteza maisha.

Licha ya serikali kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kupambana na ugonjwa huo, kazi inakuwa ngumu na maelfu ya watu wanaendelea kupoteza maisha na kuambukizwa ugonjwa huo hatari.Hali inazidi…

Added by GLOBAL on September 17, 2014 at 3:30am — 4 Comments

WAKILI WA MOYO-59

ILIPOISHIA:

 “Nashukuru sana mama, basi nikuache niwahi nyumbani.”

“Hakuna tatizo msalimie mama yako.”

“Salamu zimefika.”

Mage aliagana na mama Colin na kurudi nyumbani kwao huku dua zake zikiwa kwa Cecy asirudi hai ili aichukue nafasi ambayo aliamini ilikuwa yake hapo awali.

SASA ENDELEA...

Hakutaka…

Added by GLOBAL on September 13, 2014 at 5:30am — 12 Comments

The Last Breath (Pumzi ya Mwisho) - 70

WAKILI Lukonge anajikuta akiingia kwenye matatizo ya kujitakia baada ya kuwaua wanajeshi wa waasi na kuzidi kuwatia hasira ya kumtafuna mbichi. Lakini anapatwa na janga zito la kuanguka kwenye shimo lililokuwa likiingiza maji na baadaye kugongwa kichwani na gogo lililompoteza fahamu.

Upande wa pili Janette anaingiwa na mchecheto baada ya kukosa mawasiliano kutoka kwa wakili wao aliyeelekea kwenye msitu wa mauti, wasiwasi wake labda amekufa.…

Added by GLOBAL on September 10, 2014 at 5:00am — No Comments

TRUE LOVE -4

AKIWA kwenye ziara yake ya kikazi, mara kwa mara Rais Martin alikuwa akipiga simu ikulu kuulizia maendeleo ya mkewe ambaye alimuacha akiwa na hali ya kutatanisha.

“Mume wangu, naendelea vizuri ila nina habari njema kwako.”

“Ooh afadhali mke wangu kama unaendelea vizuri, unataka kunipa habari gani?” aliuliza Rais Martin huku akionekana kuwa na shauku kubwa.

“Wala usishtuke mume wangu kipenzi, mwenzio nime... nime...” alisema First Lady huyo lakini akashindwa kumalizia…

Added by GLOBAL on September 8, 2014 at 8:00am — 11 Comments

The Last Breath (Pumzi ya Mwisho) - 69

SAFARI ya Lukonge kuelekea msitu wa Goma inazidi kuandamwa na mikosi baada ya basi alilopanda kutokea Kalemi kuelekea Bukavu kuvamiwa na wanajeshi wa waasi mbele ya Mji wa Uvila. Katika kupambana na wanajeshi wa waasi, alifanikiwa kuwaua watano ambao waliendelea kumsaka kwa udi na uvumba.

Wakati wa kukimbia bila kutegemea anaangukia kwenye shimo lililojaa maji ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha muda huo na kupigwa na kitu kichwani na kumfanya apoteze fahamu. …

Added by GLOBAL on September 8, 2014 at 7:30am — 8 Comments

True Memories Of My Life (Kumbukumbu za Kweli za Maisha Ya Shigongo)-95

HII siyo hadithi, ni mambo yaliyonitokea kabisa maishani mwangu, nayasimulia ili kumpa mtu aliyevunjika moyo na nguvu ya kuendelea.Wiki iliyopita nilieleza jinsi nilivyoingizwa mjini na rafiki yangu wa kipindi hicho, Masumbuko Kebacho aliyenitapeli fedha zangu nyingi mno, dola laki nane na themanini na tano ambazo zilikuwa sawa na shilingi  milioni mia sita.

Huo ulikuwa ni mtaji katika biashara tuliyokuwa tunaifanya kipindi hicho ya kununua redio…

Added by GLOBAL on September 8, 2014 at 7:00am — 6 Comments

THE BLOOD STAINED DRAFT-39

Bara na Pwani ni nchi mbili ambazo zimekubaliana kuungana na kuunda jamhuri ya muungano. Watu kutoka pande hizo zote mbili wanaishi kwa amani na upendo na kushirikiana mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kiserikali.

Hata hivyo, muungano huo unaingia kwenye mgogoro mkubwa na kusababisha vurugu kubwa. Ushirikiano mzuri uliokuwepo tangu awali unavunjika na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wasio na…

Added by GLOBAL on September 6, 2014 at 6:30am — 8 Comments

WAKILI WA MOYO-58

ILIPOISHIA:

“Vipi baba?” mama yake alimuuliza.

“Safi tu,” alijibu akiwa bado ameangalia juu.

“Upo sawa baba?”

“Sipo sawa,” alijibu akiwa bado macho yake yakiangalia darini.

SASA ENDELEA...

“Kwa nini tena mwanangu?”

“Nani kampa ruhusa huyu shetani kuingia ndani?” aliuliza huku akigeuka kumtazama mama…

Added by GLOBAL on September 6, 2014 at 5:30am — 10 Comments

The Last Breath (Pumzi ya Mwisho) - 68

WAKILI Lukonge anajikuta akiingia kwenye matatizo ya kujitakia baada ya kuwaua wanajeshi wa waasi na kuzidi kuwatia hasira ya kumtafuna mbichi. Lakini anapatwa na janga zito la kuanguka kwenye shimo lililokuwa likiingia maji na baadaye kugongwa kichwani na gogo lililompoteza fahamu haijulikani amepona au amekufa. Upande wa pili Janette anaingiwa na mchecheto baada ya kukosa mawasiliano kutoka kwa wakili wao aliyeelekea kwenye msitu wa mauti, wasiwasi wake labda…

Added by GLOBAL on September 5, 2014 at 7:30am — 5 Comments

TRUE LOVE 3

Ebola, ugonjwa usio na tiba wala kinga umeikumba nchi ya Liberia na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wake. Watu wengi wanaambukizwa ugonjwa huo na ndani ya muda mfupi tu, mamia ya wananchi wanapoteza maisha. Hali ya hatari inatangazwa nchi nzima ambapo maeneo yaliyoathirika zaidi yanawekwa chini ya karantini maalum, watu wakizuiwa kuingia au kutoka bila kuwa na sababu maalum.

Licha ya serikali iliyokuwa inaongozwa na rais mwanamke, mwanamama…

Added by GLOBAL on September 5, 2014 at 4:30am — 7 Comments

THE END OF TORTURE-92

Mateso makali aliyowahi kuyapitia katika maisha yake yanabaki kuwa historia. Amelia, msichana mdogo lakini mrembo ameshateseka sana lakini sasa nyota njema imemuwakia kwenye maisha yake na kusahau yote yaliyowahi kumtokea maishani mwake.

Mateso yalianza tangu akiwa na umri mdogo sana ambapo aliwapoteza wazazi wake wote wawili, akafuatia mdogo wake na kujikuta akibaki yatima. Mateso yakaendelea kwa kipindi kirefu, likawa likitoka tatizo moja linafuata…

Added by GLOBAL on September 4, 2014 at 5:30am — 8 Comments

The Last Breath (Pumzi ya Mwisho) - 67

ILIPOISHIA:

LUKONGE anazidi kuwatia kichaa wanajeshi wa waasi baada ya kuzidi kuwaua askari wake, wakiwa na hasira wameapa kumsaka usiku na mchana mpaka wampate na kumchemsha supu. Wakati huo Lukonge hali imezidi kuwa mbaya baada ya jeraha na kusababisha kuanguka ndani ya shimo kisha kupoteza fahamu. Je, maisha ya Lukonge ndiyo yamefikia mwisho? Kuyajua yote TWENDE PAMOJA....

Askari wa jeshi la waasi waliendelea na msako mkali kumsaka Lukonge huku…

Added by GLOBAL on September 3, 2014 at 8:00am — 8 Comments

THE BLOOD STAINED DRAFT-38

Pande mbili za Bara na Pwani zilizokuwa zimeungana na kuunda jamhuri ya muungano, watu kutoka pande hizo zote mbili wakiishi kwa amani na upendo na kushirikiana mambo mbalimbali, zinaingia kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Ushirikiano mzuri uliokuwepo tangu awali unavunjika ghafla baada ya kutokea machafuko ya kisiasa kati ya pande hizo mbili na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi wasio na hatia.

Msichana mdogo, Kalunde ni miongoni…

Added by GLOBAL on September 3, 2014 at 5:00am — 10 Comments

Golden Tears (Machozi ya Dhahabu) - 30

Muigizaji mkubwa na maarufu nchini Tanzania, Goodness anahangaika kwa kipindi kirefu akisaka mtoto. Licha ya kutembea na wanaume wengi akiwa na ndoto ya kupata mtoto, muigizaji huyo anashindwa kutimiza ndoto hiyo kwani kila mwanaume anayekuwa naye, anamtumia na kumuacha.

Baada ya kutembea na mwanamuziki aliyekuwa akitikisa, Golden na kuoana naye, hatimaye Goodness anafanikiwa kupata watoto, ila tatizo ni pale anapoambiwa kwamba watoto hao…

Added by GLOBAL on September 2, 2014 at 6:30am — 3 Comments

TRUE LOVE -2

Ugonjwa wa kutisha usio na tiba wala kinga, Ebola umeikumba nchi ya Liberia na kusababisha maafa makubwa. Hali ya hatari inatangazwa nchi nzima ambapo maeneo yaliyoathirika sana yanawekwa chini ya karantini maalum, watu wakizuiwa kuingia au kutoka bila kuwa na sababu maalum.

Licha ya serikali iliyokuwa inaongozwa na rais mwanamke, mwanamama shupavu mwenye moyo wa kipekee,  Hellen Joseph, kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kupambana na ugonjwa…

Added by GLOBAL on September 1, 2014 at 7:01am — 9 Comments

The Holy Sin 42

ILIPOISHIA:

AKAMVAMIA Aidan mwilini na kuanza kufanya vilevile, akamvua shati na kukifanya kifua cha mazoezi cha Aidan kionekane, akahamia kwenye mkanda na muda mfupi baadaye, Aidan naye alikuwa amesaliwa na nguo moja tu ya mwisho. Wakakumbatiana tena huku kila mmoja akionyesha kuwa na shauku kubwa ya kilichokuwa kinataka kutokea.

SASA ENDELEA...

AKILI za kila mmoja zilikuwa zimehama kabisa eneo hilo. Hata…

Added by GLOBAL on September 1, 2014 at 7:00am — 10 Comments

The Last Breath (Pumzi ya Mwisho) - 66

LUKONGE ametonesha kidonga cha jeshi la waasi, nini hatima ya maisha yake ikiwa amewapandisha hasira baada ya kuwaua wenzao watatu na kuapa kumsaka usiku na mchana mpaka wampate na kumchemsha supu? Je, maisha ya Lukonge ndiyo yamefika mwisho? Kuyajua yote

ULIFANYIKA msako mkali kuhakikisha wanampata kwa kutawanyika wanajeshi wa waasi kila kona kumsaka Lukonge ambaye aliamini kupambana na adui zake, ndiyo njia pekee ya kuyaokoa maisha yake. Wanajeshi wa waasi…

Added by GLOBAL on September 1, 2014 at 7:00am — 17 Comments

Monthly Archives

2014

2013

2012

2011

2010

1999

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

ADVERTISE HERE

Forum

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa 2 minutes ago. 0 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by maleka sakeha on Saturday. 21 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by maleka sakeha on Saturday. 80 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by navarrohart Jun 8. 37 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by anilahsan Jun 26. 72 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Aicar Salewa May 23. 5 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by anilahsan Jul 12. 21 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

UKIMYA WA VYOMBO VYA DOLA KUTOA TAARIFA ZA MATUKIO YA MAUAJI NA UTEKAJI NI ISHARA KUWA WANAHUSIKA?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by LUPILYA GREGORY SIMON Dec 19, 2013. 7 Replies

Absalom Kibanda akiwa ICU.USIKU wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi…

Tags: UTEKAJI, NA, MAUAJI, NI, ISHARA

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service