UKUMBI WA KISLAMU

Information

UKUMBI WA KISLAMU

huu ukumbi ni wakupeana mawazo na kuelimishana mambo ya mungu munakaribishwa walio waislamu na wale ambao si waislamu mambo ya mungu hayana ubaguzi karibuni

Location: KENYA
Members: 70
Latest Activity: 9 hours ago

Discussion Forum

UMMA WA KIISLAM NA KUJENGA JUU YA MAKABURI:Kwanini ukweli huu unafichwa?

Started by Hussein Marandu. Last reply by IL-YA 9 hours ago. 5 Replies

Enyi Waislam wenye utambuzi,Asalaam alaykum.Tunaendelea na kuelimishana kuhusu fitna na upotofu wa Mawahhabi.Tunawauliza Mawahabi:Kwa nini basi wamefanya jeuri kwa kuyadharau majumba ambayo kwayo…

KUFUNGA MIKONO KATIKA SWALA NI BID'A SIO SUNNA YA MTUME (S.A.W.W) ...!

Started by IL-YA. Last reply by IL-YA on Thursday. 3 Replies

KUFUNGA MIKONO KATIKA SWALA NI…

IJUMAA MUBARAK

Started by bongo on Thursday. 0 Replies

Rabbana Waj-'alnaa Muslimayni Laka Wamin Dhurriyyatinaa Ummatam-Muslimatal-Laka Wa Arinaa Manaasikanaa Watub 'Alaynaa Innaka Antat-Tawwaabur-Rahiym.Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye…

KUJENGEA MAKABURI KTK NYUMATI ZILIZOPITA:Kwani ni ukweli huu unafichwa?

Started by Hussein Marandu May 19. 0 Replies

Waislam wenye utambuzi,Asalaam alaykum.Baadhi ya aya tukufu za Qur'an zinatufahamisha kwamba kuyaheshimu makaburi ya waumini ni jambo ambalo lilikua limeenea miongoni mwa nyumati zilizotangulia kabla…

Comment Wall

Comment

You need to be a member of UKUMBI WA KISLAMU to add comments!

Comment by bongo on April 9, 2012 at 9:58pm

 

Mama Yako Baada Ya Kifo Chake

Ndugu yangu mpendwa, jua Akurehemu Allaah ya kwamba, hakika kuwatendea wama wazazi wawili hakuishi kwa kifo chao, kwani imepokelewa Hadiyth kutoka kwa Abu Usaydi As-Sa'adiy amesema: "Wakati sisi tuko mbele ya Mtume, mara ghafla akamjia mtu mmoja kutoka kwa Banu Salimah akasema: "Ewe Mtume wa Allaah, je, kumebakia chochote katika wema kwa wazazi wangu wa kuwafanyia baada ya kifo chao? Mtume akasema: ((Ndiyo! Ni kuwaombea rahma kwa Allaah na kuwaombea msamaha na kutekeleza ahadi zao baada yao, na kuunga undugu ambao hauungwi kwa wao, na kuwaheshimu marafiki zao))

Wema kwa wazazi wawili unaendelea katika kizazi cha mwanadamu na kinachofuata baada yake, imepokelewa kutoka kwa Ibn 'Umar, amesema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((wafanyieni wema wazazi wenu, nanyi watoto wenu nao watajiheshimu))

Vile vile wema kwa wazazi wawili unazidisha umri (Akipenda mwenyewe Allaah) kwani imepokewa kutoka kwa Sahal bin Mu'aadh, ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayewatendea wema wazazi wake wawili, kheri nyingi sana ni zake yeye, Allaah Atamzidishia umri wake))

Tunamuomba Allaah Atusaidie kuwafanyia wema wazazi na kuwatii na kuwafanyia Ihsani wakiwa hai na wakiwa wamekufa, na asitufishe isipokuwa pale atakapokuwa Yu radhi na sisi, na tunamuomba Allaah Azishushe Rahma na Baraka na Amani Zake kwa Muhammad na kwa ahli zake na Maswahaba.

Comment by Marlown Mwaisanila on April 5, 2012 at 2:18am
ni kweli kuongopa tena hasa kwa mzaha ni dhambi kubwa.
Comment by bongo on March 22, 2012 at 8:04pm
Comment by Hussein Marandu on March 20, 2012 at 1:08pm
FIKRA ZA KIWAHHABI NI KUYAKUFURISHA MADH-HEB NA KUPANDA MBEGU YA CHUKI NA UTENGANO MIONGONI MWA WAISLAM.
Enyi Waislam wenye utambuzi,
Asalaam alaykun.Mmesoma nasiha za mara kwa mara kutoka kwa ndugu yetu Bongo.Safi sana.Namsihi ndugu yetu huyu kwamba mtandao anaotoa mada zake alhidaaya.com ni mtandao wa Mawahhabi ambao lengo lao ni kuwapotosha Waislam,kuleta chuki na utengano miongoni mwa Waislam na kuwakufurisha wote ambao sio Mawahhabi.Bongo na wapambe wake ni muhimu sana wawaambie Waislam asili ya dini yao,wametoka wapi,walipotea wapi na wafanye juhudi gani sasa ili wote tushikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu na wala tusifarakiane.Na wanaogopa kurudi kwenye tarekh maana tarekh itawaumbua.Ni bahati mbaya sana kwamba Bongo na wapambe wake wamenasa ktk fikra potofu za kiwahhabi na kua wafuasi wa Muawiyyah na Yazid na inshallah Mwenyezi Mungu ni Mlipaji Bora kabisa.
Naam maneno yangu haya yana ushahidi.Nitamchukia na kumpinga sana yeyote,kwa ushahidi madhubuti sio ushahidi blaa blaa na ninapofanya hivyo sijali yeyote huyo ni bongo,masonga,alhidaaya.com,Muawiyah,Yazid,Abubakar au hata Imam Ali(a.s) mradi tu nautetea Uislam Mtukufu,Mtukufu Mtume(s.a.w.w) na Ahlul Bayt Rasulullah(s.a.w.w) na ikiwa kufanya haya ni kua rawafidha basi mimi Hussein Marandu ni rawafidha mkubwa.
Ewe msomaji mtukufu,
Kipo kitabu kiitwacho "AS-HIATU-WA AT-TASHAYUU" kilichotungwa na Mpakistani mwenye chuki ambae ni miongoni mwa wanaofadhiliwa na Mawahhabi,jina lake ni Ihsan Ilahi Dhahir na kimechapwa Saudia.Na ndani yake mtungaji anazitupa tuhuma na uzushi dhidi ya Ushia,na anadai kwamba yeye anaeleza kutokana na vitabu na rejea za Mashia.
Kwa mfano,utaona ktk uk wa 20 wa kitabu hicho,anataja neno la Al-Mar-hum Al-Ustadh Mheshimiwa Sheikh Muhammad Hussein Al Mudhafar,kisha analisherehesha kufuatana na vile apendavyo yy na vile nafsi yake inayoamrisha maovu inavyomtuma.
Tunaweka wazi neno hilo pamoja na sherhe ya Wahhabi huyu ili uone mwenyewe jinsi Mawahhabi waliofilisika kwa dalili,wanavyotegemea maneno ya tuhuma,uzushi na uongo dhidi ya Shia.Mar-hum Al-Mudhafar anasema:
"Fakanatid-Daawatu Littashayui Liabil-Hassan Alayhis-Salaam Min Sahihir-Risalat Salallahu Alayhi Waalihi Wasallam Tamshi Minhu Janban Liyanbi Maad-dawat Lish-Shahadatayn"
Tafsir Yake:
Mwito kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kumfuata Abul Hassan Ali(a.s) ulikua ukienda sambamba na mwito wa Shahada mbili.
Na maana ya maneno yake haya ni kwamba:
Ushia haukuzalikana kutokana na hali ya kimazingira wala sio madhheb yaliyoanzishwa baadae,bali ni Madh-heb ya asili ambayo chanzo chake kinaanzia kwa mwenyewe Mtume Muhammad (s.a.w.w),kwani Mtume (s.a.w.w) alikua akilingania watu juu ya Uimam wa Amirul-Muuminina Ali(a.s) sambamba na wito wa Shahada mbili.
Kisha Wahabi huyu muovu anayawekea Taaliq maneno ya Sheikh Mudhafar na anasema:
"Hakika Mtume(s.a.w.w)[kwa mujibu wa madai ya Mudhafar] alikua akimfanya Ali kua ni mshirika wake ktk Unabii wake na ujumbe wake"!!!
iwapo mwandishi huyu sio mtumwa wa matamanio yake yenye chuki na mwenye kufadhiliwa na Mawahab, na iwapo ni mchunguzi wa Itikadi za Kiislam za Kishia angesema na kusimamia Haki.
Uk 49 anatuhumu Ushia kwamba umepokea fikra zake kutoka kwa Abdallah Bin Sabaa aliyezalikana kutoka kwa Myahudi wa Yemen,na anavyoitakidi Tabari ni kwamba Abdallah Bin Sabaa alidhihirisha Uislam na kuficha Uyahudi na mapenzi yake kwa Imam Ali(a.s) aliyafanya kifuniko cha kueneza fikra zake.
Mwandishi huyu wa Kiwahhabi anategemea mambo aliyoyapokea Tabari kuhusu uzushi huu,Amma sanad ya riwaya ambayo Tabari anaielezea ni kama ifuatavyo neno kwa neno:
"Aliniandikia As-Sariyyu kutoka kwa Shuaib,kutoka kwa Seif,kutoka Atiyyah nae toka kwaYazid Al-Faq-Asi:Abdallan Bin Sabaa alikua Myahudi ktk watu wa San-aa...."[vile vile ameipokea riwaya hii Ibn Khaladun Al-Magharib na Ibn Kathir Ash-Shami na walio mfano wa Tabar miongoni mwa maadui wa Ahlul-Bait].
Sasa tunaiweka riwaya hii kwenye meza ya uchunguzi.
Kwa mtazamo wa haraka ndani ya vitabu vya elimu ya rijali (ambavyo vimeandikwa na wanachuoni wa Kisunni) vitatutosheleza kufahamu hali za wapokezi hawa:
1)As-Sari sawa sawa akiwa ni As-Sari Ibn Ismail Al-Kufi au As-Sari Ibn A'sim aliyekufa mwaka 258 kila mmoja wao ni miongoni mwa waongo na wazushi.
Tazama:
a)Tahdhibut-Tahdhib cha Ibn Hajar Juz 3 uk 46
b)Tarekh Al-Khatib Juz 1 uk 193
c)Mizanul-Itidal Juz 1 uk 37
d)Lisanul Mizan Juz 3 uk 13
2)Shuaib Ibn Ibrahim A-Kufi:Majhul[Hatambulikani hali yake]Tazama:a)Mizanul-Itidal Juz1 uk 447
b)Lisanul-Mizan Juz 3 uk 145.
Haya ndiyo mategemeo ya uzushi na uongo wa Mawahhabi dhidi ya Ushia.Hawa ndio watetezi wa Tawhid na Sunna.Wao ni wapenzi na watetezi wa Muawiya na Yazid wauaji wa Bwana wa Vijana wa Peponi Imam Hussein(A.S) na watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w)Na malipo mema yapo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Comment by bongo on March 13, 2012 at 8:25pm

Muenzi Mke Wako


 

Khutbah Kutoka Kwa Shaykh 'Abdullaah 'Adhamiy

Imefasiriwa na Iliyaasa bint Maulaana

 

 

Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako mpenzi.

Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.

Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona ni macho yake. Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu wake mzima.  

Kielezo bora kabisa ambacho mimi binafsi nishawahi kusoma kinafafanua ukaribu wa wanandoa juu ya wao kwa wao na kielezo hicho kipo katika aya ya Qur-aan ambayo inasema:

((Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao)) [Al-Baqarah 2:187].

Na Kweli, wanandoa ni kama vazi juu ya wao kwa wao kwa sababu wanapeana ulinzi, liwazo, kinga (stara), msaada (tegemeo), na mapambo ambayo vazi linampa mtu. Hebu jaribu kufikiri msafara wakati wa siku za baridi kwenda sehemu kama vile Alaska bila ya kuwa na nguo! Wanandoa wetu wanatupa kiwango kile kile cha faraja (liwazo), ulinzi, na msaada  katika msafara wa maisha yetu katika dunia hii kama vile nguo itakavyofanya katika msafara wa Alaska.

Mahusiano baina ya wanandoa ni ya kustaajabisha kabisa katika mahusiano yote ya kibinaadamu: Idadi ya mapenzi na mahaba, undani na ukaribu, huruma na imani, amani na utulivu ambao unajaza nyoyo za wanandoa ni jambo lisiloelezeka kwa wepesi. Ufafanuzi pekee wa mantiki ambao unaweza kuelezeka juu ya haya mastaajabu makubwa katika hisia zote za kibinaadamu ni kwamba: Ni kitendo cha Allah Subhanahu wa Ta'ala, ((Na Mwenyezi Mungu Amekuumbieni wake [na wenza katika jinsi yenu])) [An-Nahl 16:72]

Mola wetu tu Allah Subhanahu wa Ta'ala katika katika Utawala Wake usio na upeo wa huruma Yake  isiyo na mipaka  na Hekima Yake adhimu Anaweza kujenga na kuzididimiza katika akili hizi hisia za kustaajabisha na za kubarikiwa katika nyoyo za wanandoa. Kwa kweli Allah Subhanahu wa Ta'aala Anawakumbusha wale ambao wanatafuta ishara Zake katika ulimwengu huu kwamba hisia hizi katika moyo wa wanandoa ni katika ishara Zake ambazo zinatakiwa zimuongoze mwanaadamu katika kuwepo Kwake kama Alivyosema katika Qur-aan, (Na katika Ishara zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri." [Ar-Ruum 30:21]

Lakini Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta’aala Anajua kwamba moyo wa binaadamu sio kitu ambacho kiko tuli, wakati mwengine huwa dhaifu na wakati mwengine huwa na nguvu. Hisia zinaweza kubadilika na hubadilika pindi wakati unavyosogea. Mapenzi yanaweza kufifia na kupayuka mbalini. Mshikamano wa ndoa unaweza kuwa dhaifu kama haujahudumiwa vizuri. Furaha katika ndoa haiwezi kudharauliwa; furaha ya kuendelea inahitaji utowaji wa daima kutoka pande zote. Ili mti wa mapenzi ya ndoa ubaki hai na kuendelea kuishi, udongo lazima udumishwe, uhifadhiwe, umwagiwe maji na ulelewe.

Kumbuka kwamba Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipata nafasi ya kwenda kwenye majangwa na kushindana mbio na mke wake Bibi 'Aishah. Bibi 'Aishah alimshinda Mtume lakini baadae aliponenepa, Mtume alimshinda Bibi 'Aishah. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimchukua mkewe kwenda kuwatazama vijana wa Ki-Ethiopia wakicheza michezo ya utamaduni wao. Maonyesho ya hisia yanahitajika kuweza kuufanya mshikamano wa ndoa usifanye kutu na kuoza. Kumbuka kwamba utapata thawabu kutoka kwa Allah (Subhanahu wa Ta'aala) kwa hisia zozote unazomuonyesha mkeo kama Mtume   (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyosema: ((Mmoja wenu atapata thawabu kwa chochote ambacho atafanya ili kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu hata kwa tonge analomlisha mkewe))

Kamwe usidharau umuhimu wa vitu vidogo vidogo kama vile kuweka chakula kwenye mdomo wa mkeo, kumfungulia mlango wa gari, na hali kadhalika. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasogeza goti lake kwa mkewe amkanyage kuweza kumpanda ngamia.

Jaribu kutafuta wakati ili nyote wawili muweze kuswali pamoja. Kuuimarisha uhusiano kati yenu na Allaah (Subhanahu wa Ta'aala) ni hakikisho kubwa kuwa uhusiano wenu wa kindoa utabaki madhubuti. Kuwa na amani kati yenu na Allah (Subhanahu wa Ta'ala)  daima kutapelekea ndani mwenu kuwa na amani zaidi.

Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapa habari nzuri (aliwabashiria) wanandoa wanaoamka usiku kuswali pamoja. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anamsisitiza mwanandoa anayeamka mwanzo amuamshe mwenzake, japo kummwagia maji katika uso wake. 

Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongea nae, mchekee, tafuta ushauri wake, muulize juu ya mawazo yake, tumia wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Wabora katika nyinyi ni wale ambao ni wabora kwa wake zao))

 Mwishowe, ni kawaida kwa wanandoa kuahidi kuwapenda na kuwaheshimu wanandoa wenziwe mpaka mauti yawatenganishe. Naamini kwamba ahadi hii ni nzuri au ni bora kabisa, lakini haitoshi! Haitoshi kumpenda mkeo tu. Lazima upende anachokipenda pia. amilia yake, anaowapenda yeye uwapende pia. Usiwe kama mwenzangu mmoja ambaye hakufurahiwa kuja kwa wazazi wa mke wake kukaa kwa wiki chache. Alimwambia wazi mkewe “Mimi siwapendi wazazi wako”. Bila ya kusita mkewe alimtazama machoni kwa hasira na kusema, “Na wako pia siwapendi”.

Mapenzi yasiishe na pia tunaamini kuna maisha baada ya mauti ambapo wale ambao walifanya wema katika dunia hii wataungana na wanandoa wenzio ((Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo)) [Az-Zukhruf 43:70] Pia wataungana na watoto wao.

Na mfano bora katika mintarafu hii itakuwa ni Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye mapenzi yake kwa Bibi Khadiyjah, mkewe aliyeishi naye kwa miaka 25 yalisogea mpaka kwa wale aliowapenda Khadiyjah; mapenzi yake haya yaliendelea hata baada ya kufa Bibi Khadiyjah. Ilikuwa miaka mingi baada ya kifo cha Bibi Khadiyjah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakumsahau na kila panapochinjwa mbuzi katika nyumba yake basi hutuma kifurushi kwa familia ya Bibi Khadijah na marafiki zake na kila akihisi kuwa mgeni  anayegonga mlango ni Dada ya Khadijah aitwaye Hala, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alikuwa akiomba huku akisema, “Ewe Mwenyezi Mungu Jaalia awe ni  Hala

Comment by Hussein Marandu on March 10, 2012 at 11:26am
MAPINDUZI YA KIISLAMU NA HUJUMA ZA KIWAHHABI.
Ewe Muislam mwenye utambuzi,
Asalaam alaykum.
Kwa hakika Mapinduzi ya Kiislam nchini Iran,yalileta mshituko mkubwa ktk ghuba,na kuzisononesha tawala zote zilizoko sehemu hiyo na hasa hasa zinazohusiana na mataifa makubwa na kuyategemea kwa kila hali,na kwa upande mwingine madola hayo ya kikoloni yanazitegemea nchi hizo na miongoni mwa tawala hizi ni ule utawala wa Kiwahhabi unaotawala nchi kubwa miongoni mwa nchi za Kiislam,nchi ambayo inasifika kwa utajiri mkubwa wa asili na inanufaika kwa hali maalum ya kijiografia.
Basi ukoloni mbaya na vibaraka wake na watendaji wake wakiongozwa na walinganiaji wa Kiwahhabi wamekusudia kupinga mapinduzi ya Kiislam na kimbunga chake kwa njia mbalimbali,miongoni mwa upinzani huo ni kuzusha wasiwasi ndani yake na kuwasha mioto ya vita dhidi yake na kulazimisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Mapinduzi hayo.
Na njama zote hizi za upinzani dhidi ya mapinduzi ziliposhindwa,wakakusudia kuleta picha mbaya ya utamaduni wa mapinduzi na kuondosha Maf-humu yake na kuuzushia uongo na kuupakazia uzushi ili kuwazuia watu kufuata muongozo wake na kumfuata kiongozi wa mapinduzi hayo.
Kwa hakika njama hii ya kiuadui dhidi ya utamaduni wa mapinduzi ya Kiislam,inabainika ktk mambo yafuatayo:
1)Kueneza matangazo na magazeti aina nyingi ktk nchi mbalimbali za ulimwengu ili kuzungumzia dhidi ya mapinduzi na kufanya ushawishi dhidi yake na kuonyesha sura mbaya ya utamaduni wake halisi.
2)Kuchapisha vijitabu na vitabu vingi mno kuhusu utamaduni huo kwa kupitia mikono ya watu na waandishi ambao wameuza nafsi zao na hawajali isipokua mlo wao na pengine vyeo vyao vya kidunia wakiongozwa na yule muongo mkubwa Ih-Sa'an ilahi Dharir( marehemu) ambae ni miongoni mwa watu waliokua wanapata mali nyingi kutoka Saudia.
Mtu huyu alisimama kidete kwa nguvu zake zote na kwa kila kitu ambacho Saudia inakitoa ili kutoa picha mbaya ya taaluma ya mapinduzi miongoni mwa Waislam.
Na huyu bwana alikua maskini kwa kila kitu hata ktk madai yake kua anayafahamu madh-hebu ya Shia Imamiyyah,basi anachanganya na kuvuruga na wala hapambanui baina ya Asili na na Far-i.Wala baina ya Aqida na Riwaya,na anatoa ushahidi kwa kutumia riwaya kua eti ndiyo madh-hebu ya Shia yalivyo.
Yapo mengi zaidi ya hayo ktk uongo wake na uzushi wake na natija mbovu atoazo.
3)Kuyaeneza Madh-hebu ya Kiwahhabi miongoni mwa vijana ktk eneo hilo kwa njia mbalimbali huku wakibainisha wazi kua Mawahhabi ndio Waislam na kwamba wao ndio wanaompwekesha Mwenyezi Mungu na ndio wanaoitumia Qur'ani na Sunna kwa usahihi,na wasiokua wao ni makafiri!!!Allah Mtukufu Ndiye
Mjuzi Zaidi(Itaendelea)
Comment by bongo on March 9, 2012 at 5:26pm

Kila Kitu Kinamsujudia Allaah سبحانه وتعالى, Je,Wewe Mwana Aadam?

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ

 وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩

 

((Je! Hawavioni vitu Alivyoviumba Allaah, - vivuli vyao vinaeleea kushotoni na kuliani, kumsujudia Allaah na vikinyenyekea?)) ((Na vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi, tangu wanyama mpaka Malaika, vinamsujuidia Allaah, na wala havitakabari))  ((Vinamkhofu Mola wao Aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa)). [An-Nahl: 48-50]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hana mshirika wala msaidizi bali Yu Pekee Naye Ndiye Apasaye kuabudiwa. Viumbe vyote vinapasa kumsujudia Yeye, hata vitu vyote Alivyoviumba vinamsujudia   vikitaka visitake:

((وَلِلّهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلالُهُم بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ))

((Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Allaah tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni)). [Ar-Ra'd: 15].

 

Na katika Hadiyth ifuatayo,

 

عن أبي ذَرٍّ - رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((أَتَدْرِي أَيْنَ تَذْهَب هَذِهِ الشَّمْس ؟)) قُلْت اللَّه وَرَسُوله أَعْلَم. قَالَ : ((فَإِنَّهَا تَذْهَب فَتَسْجُد تَحْت الْعَرْش ثُمَّ تَسْتَأْذِن رَبّهَا فَيُوشِك أَنْ يُقَال لَهَا اِرْجِعِي مِنْ حَيْثُ جِئْت))

Imetoka kwa Abu Dharr (Radhiya Allaahu ‘anhu)   kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Unajua jua hili linakwenda wapi?)) Nikasema: "Allaah na Mjumbe Wake Wanajua". Akasema: ((Linakwenda na kusujudu chini ya 'Arsh, kisha linaomba idhini ya Mola wake, na karibuni litaambiwa: Rudi ulikotoka)). [Muslim].

 

 وعن ابن عباس قال: "جاء رجل فقال: يا رسول الله، إني رأيتني الليلة وأنا نائم، كأني أصلي خلف شجرة، فسجدتُ فسجَدَت الشجرة لسجودي، فسمعتُها وهي تقول: ((للّهُـمَّ اكْتُـبْ لي بِهـا عِنْـدَكَ أَجْـراً ، وَضَـعْ عَنِّـي بِهـا وِزْراً ، وَاجْعَـلها لي عِنْـدَكَ ذُخْـراً ، وَتَقَبَّـلها مِنِّـي كَمـا تَقَبَّلْتَـها مِنْ عَبْـدِكَ داود)). قال ابن عباس: فقرأ  النبي صلى الله عليه وسلم سجدة ثم سَجَد، فسمعته وهو يقولُ مثلَ ما أخبره الرجل عن قول الشجرة.  رواه الترمذي، وابن ماجه، وابن حبّان في صحيحه

Na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa)  amesema: "Mtu moja alikuja na kusema: "Ee Mjumbe wa Allaah, nilijiona katika ndoto jana usiku nikiswali nyuma ya mti. Niliposujudu na mti ukawa unasujudu. Kisha nikausikia unasema: ((Ee Allaah,  Niandikie Kwako kwa sijda hii malipo, na Nifutie kwayo madhambi, na Ijaalie kwangu mbele yako ni akiba, na Nikubalie kama ulivyomkubalia mja wako Daawuwd)) Ibn 'Abbaas akasema: "Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   akasoma Aayah inayotaja kusujudu kisha akasujudu na nikamsikia akisema maneno hayo hayo aliyosimulia mtu yaliyotajwa na mti."  [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake].

 

Na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ah   Anasema:

 

((أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَاب))

((Je! Huoni kwamba vinamsujudia Allaah viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu)). [Al-Hajj: 18].

 

Aayah hiyo mwisho inasema kuwa ((Na wengi imewastahiki adhabu)) kwa maana kwamba wale ambao hawataki kusujudu. [Ibn Kathiyr 6:540].

 

Basi ndugu Muislamu tunatumai kuwa hutokuwa miongoni mwa wanaostahiki adhabu. Hivyo timiza Swalaah zako tano za fardhi zipasavyo kuswaliwa kwa kuzidumisha na kuziswali kwa wakati wake. Kisha utakapokuwa umezidumisha Swalaah zako tano basi jiongozee kuswali Swalaah za Sunnah uzidi kumnyenyekea Mola wako na kupata fadhila nyingi za kusujudu na za kuswali Swalaah za Sunnah. Na pia kila unaposoma Aayah iliyo na Sajdah, pinduka umsujudie Mola wako Mtukufu.

Comment by Hussein Marandu on March 8, 2012 at 4:47pm
MSIMAMO WA MAWAHHABI NA QADHIA YA TAUHIDI -2-
Ewe Muislam mwenye utambuzi.
Asalaam alaykum,
Utakapolinganisha yale yaliyonakiliwa kutoka kwa As-Habul-Hadith kuhusu Tauhid ya Mwenyezi Mungu na kumtakasa kwake utastaajabu,kwani Imam Al-ash-ari (mawahhabi hawawafuati Maimamu wanne wa Kisunni)amenakili toka kwao kwamba,maana ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu ktk kuumba ni kwamba: "Maovu ya waja anayaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu na kua matendo ya waja anaeyaumba ni Mwenyezi Mungu na waja hawawezi kufanya chochote"(Tazama: Maqa'latul-Islamiyyin uk 321)
Bila shaka Ibn Taimiyyah na wale walioko kama yeye wanajisifu wenyewe kua ni Ahlul-hadith na wanaitafsiri Tauhid inayohusu kuumba kwa namna hii.Basi ikiwa Mwenyezi Mungu ndie anayeumba maovu ya waja, na waja hao wakawa hawana walichokifanya ktk maovu hayo,si kwa uwezo wao wala kwa kuiga, basi ni kwanini Mwenyezi Mungu awaadhibu?
Nawe msomaji unatambua kwamba Tuhidi inayohusu kuumba haimaanishi kama walivyoieleza Ahlul-Hadith,na kabla na baada yao waliyasema kama hayo Jabriyyah na Ibn Taimiyyah na wafuasi wake.
Bali maana yake ni kwamba:
Muumba mwenye kujitosheleza na mtendaji asiyehitaji kitu chochote ni Mwenyezi Mungu Mtukufu.Lkn wako watendaji wanaotenda kwa idhini Yake na wanaumba kwa amri Yake na husimama na kukaa kwa amri uwezo Wake na nguvu Zake,hivyo basi mtu analo jukumu lake kutokana na matendo yake na kazi yake "Kila nafsi itafungika kwa yale iliyotenda"Tazama: Qur'an 74:38.
WANACHUONI WA KIWAHHABI WANAJIPENDEKEZA KWA WATAWALA:
Tunaona kwamba wanachuoni wa Kiwahhabi nchini Saudia na sehemu zingine wanajipendekeza kwa watawala na Makhalifa wajeuri,wanajaribu kuyatakasa matendo ya dhulma ya watawala hao na misimamo yao ya kijeuri,na wanajitahidi kutoa kibali cha kisheria kwa kila kinachotokana na watawala wao na wenye mamlaka juu yao awe mwema au muovu.
Na hilo si jambo la ajabu kwa Mawahhabi kwani wao Mawahhabi ndio wanaona kua kusali nyuma ya kila Imam,awe mwema au muovu,sala inasihi,na kuwaombea wema viongozi wa waislam ni faradhi,na kuwapinga wanapopotoka ni haram!(Tazama: Maqalatul-Islamiyyah uk 322---na hii ni itikadi ya ahlul-hadith na Ibn Taimiyyah na wafuasi wake ktk kundi hili)
Wanaichukuliaje kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kama alivyoinakili Mjukuu wake Hussein bin Ali(a.s) "Abus-Shuhadaa" pale aliposema:
"Enyi watu,hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)amesema;mtu yeyote atakayemuona mtawala muovu anaehalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu,mwenye kutengua ahadi ya Mwenyezi Mungu,mwenye kwenda kinyume cha Sunna ya Mtume(s.a.w.w),anawatendea uovu na uadui waja wa Mwenyezi Mungu,kisha mtu huyo akaacha kumkataza kwa kitendo au kauli basi Mwenyezi Mungu Atakua na haki ya kumuingiza motoni mtu huyo" (Tazama: Tarikh At-Tabari Juz 4 uk 304--matukio ya mwaka 61.)Mwenyezi Mungu amesema:
"Wala msiwategemee(mkawa pamoja nao) wale wanaodhulumu usije kukupateni moto"(Tazama: Qur'an 11:113)Allah Ndie Mjuzi Zaidi(Itaendelea)
Comment by Hussein Marandu on March 8, 2012 at 1:38pm
MSIMAMO WA MAWAHHABI KTK QADHIA YA TAUHIDI -1-
Ewe Muislam mwenye utambuzi,
Asalaam alaykum,
Cha ajabu (na midhali upo hai utaona maajabu zaidi) ni kwamba Uwahhabi unatokana na fikra ya Sheikh mpotofu aitwaye Ibn Taimiyyah.Ktk kitabu chake Maj-mu'a 'Tur-Rasailil-Kubra,al-A'Qidatul-Wasitiyah uk.309 na 401 anasema:"Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu ya mbingu yake kwenye arshi yake,yuko juu ya viumbe wake"
Na amesema tena:"Mola wetu hushuka mpaka kwenye mbingu ya dunia kila siku inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku kisha husema; nani ataniomba (saa hizi) nami nitamkubalia (maombi yake) nani ataniomba nami nitampa,nani atanitaka msamaha nami nitamsamehe"
Haya ndiyo maarifa ya mtu huyu mpotofu Ibn Taimiyyah na huku ndiko kumtakasa kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu.Kutokana na kusema kwake hayo,inajulisha wazi kabisa kua yeye anaitakidi kua Mwenyezi Mungu anao mwili na anapatikana mahala fulani.Na ameyasema haya huyu mtu mpotofu kutokana na kung'ang'ania kwake dhahiri ya aya na hadithi za Mtukufu Mtume(s.a.w.w) bila ya kuzitafakari kwa undani aya zilizokuja kuhusu maudhui hiyo, na bila ya kufanya uhakiki ktk isnad za hadithi na madhumuni yake.
basi iwapo haya ndiyo maoni ya mwalimu wa Mawahhabi,basi itakuwaje hali ya watu wanaoramba vikombe vyake,na wanaokaa ktk meza zake kama kina Ibn Qayyim na Muhammad Bin Abdul Wahhab(hapa wapo pia akina masonga,bongo na wenye alhidayyah.com pamoja na wenye kr-hcy.org).Eti hawa nao wanataka wawe ni waalimu wa Tauhidi na walinganiaji wa Tauhidi.
Hii ndiyo itikadi ya Mawahhabi kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu.Iwapo tutataka kuzipima fikra hizi,basi tunawajibika kulinganisha kati ya maelezo hayo na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) kuhusu Tauhidi,kisha tuone ni lipi kati ya makundi haya mawili lenye haki ya kufuatwa:
Jee,ni yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwamba yeye ana mwili na anakaa upande fulani na anateremka mpaka mbingu ya dunia ndie wa kufuatwa au ni yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwa kusema:
"Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu ambae hawafikii kikamilifu sifa zake wenye kuzisema,wala hawazidhibiti neema zake wenye kuhesabu,na wala hawatekelezi ipasavyo haki yake wenye kujitahidi,Mwenyezi Mungu Mtukufu ambae fikra hazimfikii hata ziende umbali kiasi gani,wala akili hazimfikii japo ziende ndani kiasi gani,ambae sifa zake hazina mpaka,wala hakuna maneno yatakayoeleza sifa zake kikamilifu.Na yeye hana wakati uliohesabiwa wala muda uliopangwa.Mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa fikra zake atakua kamfanyia mwenza,na mwenye kumfanyia mwenza atakua kamfanya wawili.Na mwenye kumfanya wawili basi atakua kamgawa.Na mwenye kumgawa hakumjua,na asiyemjua atamuashiria na mwenye kumuashiria atakua kamuwekea mipaka,na mwenye kumuwekea mipaka atakua kamfanya kua zaidi ya mmoja,na atakaeuliza yuko ktk kitu gani basi yeye atakua kamuweka ndani ya kitu,na atakaemuuliza kua yuko juu ya kitu gani basi yeye atapafanya mahala pengine pote kua Mwenyezi Mungu hayupo.Yeye yupo lkn si kwamba hapo kabla hakuwepo,Yupo pamoja na kila kitu lkn si kwa kuambatana nae yu mbali na kila kitu lkn si kwa kuondoka"Tazama: Nahjul-Balagha Khutba ya Kwanza.Allah ni Mjuzi Zaidi (Itaendelea)
Comment by bongo on March 2, 2012 at 3:03pm

SWALAH - 1 - Maana Ya Swalah Na Kuwajibika Kwake



 

Maana Ya Swalah Kilugha
 
Ni du'aa kama Anavyosema  Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
 ((خُذْمنْ أَمْوَلِهمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ و تُزَكِّيهِمْ بِهَا و صَلِّ عَلَيْهِمْ إِنَّ صلواتك سَكَنٌ لَّهُمْ وَ آللّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ))
((Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele ya Allaah) na uwaombee du’aa. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu na Allaah ni Mwenye kusikia Mwenye kujua)) [At-Tawbah: 103]
 Hadiyth ifuatayo inathibitisha pia maana hiyo:
 
عن أبي هريرة -رضي الله عنه- قال: قال رسول الله -صلى الله عليه وسلم: ((إذا دعي أحدكم فليجب فإن كان صائمًا فليصلِّ و إن كان مفطرًا فليطعم)) أخرجه مسلم         
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Akialikwa mmoja wenu aitike (mwaliko), ikiwa amefunga  (Swawm) awaswalie (yaani aombe (du'aa kwa waliomualika), akiwa hakufunga basi ale (chakula)))[Muslim]  [Inamaanisha awaombee du'aa ya maghfirah, baraka na kheri)
 
Swalah kutoka kwa Allaah ni sifa njema na kutoka kwa Malaika ni du'aa kama Anavyosema:
((إنَّ اللَّهَ وَ مَلاَئِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى آلنَّبِيِّ يَا أَيُّهَا آلَّذِينَءامَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَ سَلِّمُوا تَسْلِيمًا))
((Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabii. Enyi mlioamini! Mswalieni (muombeeni) na mumsalimu kwa salamu)) [Al-Ahzaab: 56]
Abu 'Alyah amesema: Swalah ya Allaah ni kumsifu mja kwa Malaika Wake na Swalah ya Malaika ni du'aa.
Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Wanawaswalia" maana wanawabarikia"  
Vile vile Swalah kutoka kwa Allaah ni Maghfirah (msamaha) au Baraka. Swalah kwa maana ya Maghfirah nikutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
 ((أُوْلئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَواتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَ رَحْمَةٌ وَ أُوْلئِكَ هُمُ آلْمُهْتَدُونَ))
((Hao juu yao zitakuwa maghfira zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka))[Al-Baqarah: 157]
Na kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alisema:
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى آل أَبِي أَوْفَى
Allahumma Swalli ‘alaa Aali Abi Awfiy Akimaanisha ‘Ee Mola wangu wasamehe jamaa wa Abu Awfiy’.  
Hivyo hapa Swallah ina maana ya Maghfirah (msamaha).
 
 
 
Maana Swalah Kishari'ah
 
Ni kumuabudu Allaah kwa kauli na vitendo maalumu na khaswa (pekee) vinavyoanza na Takbiyr (Allaahu Akbar) na kumalizika na Tasliym (kutoa salam).
Na imeitwa Swalah kwa sababu inahusiana na du'aa katika kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) tunaposimama, tunaporukuu, tunaposujudu na tunapokaa, hivyo Swalah nzima ni du'aa.
 
 
Hukumu Ya Swalah
 
Swalah ni fardhi kwa kila Muislamu mwenye akili timamu, aliyebaleghe kutokana na dalili kutoka katika Qur-aan:
   ((وَمَا اُمِرُواْ إِلاَّ لِيَعْبُدُواْ آللّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ آلدِّينَ حُنَفَآءَوَ يُقِيمُواْ آلصَّلاَةَ وَ يُؤْتُواْ آلزَّكَاةَ وَ ذَلِكَ دِينُ آلْقَيِّمَةِ))
((Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swalah, na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti))[Al-Bayyinah: 5]
   ((إِنَّآلصَّلاَةَ كَانَتْ عَلَى آلْمُؤْمِنِينَ كِتابًا مَّوْقُوتًا))
((Kwani hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu)) [An-Nisaa: 103]

Ama katika Sunnah ni kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomtuma Mu'aadh Bin Jabal (Radhiya Allaahu) kupeleka ujumbe Yemen kwa kumwambia: ((…na wafundishe kwamba Allaah Amewafaridhisha Swalah tano kila siku…)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Vile vile,
  عبدالله بن عمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( بُنِـيَ  الإِسْلاَمُ علـى خَمْسٍ: شَهادَةِ أنْ لا إِلٰهَ إلا الله وأنَّ مُـحَمَّداً رَسُولُ الله وإِقامِ الصَّلاَةِ وإِيتاءِ الزَّكاةِ وَحَجِّ البَـيْتِ وَصَوْمِ رَمَضَانَ)) البخاري
Kutoka kwa 'Abdullaah ibn 'Umar ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Uislamu umejengeka kwa matano; Kushuhudia (na kukiri kwa moyo)  kwamba hakuna Mola Apasaye kuabudiwa (kwa haki) isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allaah na kuswali (Swalah tano), kutoa Zakaah, kuhiji katika Nyumba (Makkah) na kufunga (mwezi wa) Ramadhaan)) [Al-Bukhaariy]
Kuna Aayah na Hadiyth nyingi zinazothibitisha kuwajibika kwa Swalah. Ama mwanamke mwenye hedhi na aliye katika nifaas hawawajibiki kuswali kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  
 
  أليس إذا حاضت المرأة لم تصل ولم تصم ؟  -متفق       
((Kwani sio kweli kwamba mwanamke anapokuwa katika hedhi haswali wala hafungi?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
 

Members (70)

 
 
 


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

Sili Silali liked GLOBAL's blog post PSI YATOA SEMINA YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KATIKA MABAA NA VILABU YA POMBE JIJINI MBEYA
2 hours ago
Theddy Jacob liked GLOBAL's blog post SETH AFUNGUKIA PENZI LA LULU, KANUMBA
4 hours ago
Saleh Jadid Saleh commented on IL-YA's blog post Dubai:House girl,achanganya mkojo wake na chakula cha mwajiri wake!.Huko Singapore nako wembe ni ule ule!
"Kumbe ww Ilya Upo Iran? nilikuwa sijui mpaka nimesoma profile yako, nakuhurumia kwa kusema uongo…"
8 hours ago
asha liked GLOBAL's blog post Mapenzi ni fursa, iheshimu kwa maana haiji mara mbili
8 hours ago
IL-YA replied to Hussein Marandu's discussion UMMA WA KIISLAM NA KUJENGA JUU YA MAKABURI:Kwanini ukweli huu unafichwa? in the group UKUMBI WA KISLAMU
"Dada Saumu,@ kuhusu kupotea kaburi la mama yako,nakupa pole sana kwa hilo,na hilo limetokana na…"
9 hours ago
chiya left a comment for Jazihina Jaziu
"hi jazihina vipi hali sorry nimechelewa kukujibu  "
10 hours ago
chiya left a comment for chiya
"hi vipi hali sorry nimechelewa kukujibu "
10 hours ago
kajerekani commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Gold digger

"hii ni kali ya mwaka"
11 hours ago
Matata Mpili shared GLOBAL's blog post on Facebook
12 hours ago
Matata Mpili shared GLOBAL's blog post on Facebook
12 hours ago
Matata Mpili shared GLOBAL's blog post on Facebook
12 hours ago
arthur moore commented on IL-YA's blog post Dubai:House girl,achanganya mkojo wake na chakula cha mwajiri wake!.Huko Singapore nako wembe ni ule ule!
"Ooh!! asante IL-YA kwa hiyo habari kweli waarabu sio watu wengi wao hawana utu kabisaa na watoto…"
12 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website