Ni jambo lisilopingika kwa mtanzania yeyote mwenye akili kuwa umasikini wetu tulio nao kwa sasa sio wa mali bali ni wa viongozi. Maana kama ni mali Tanzania tuna mali nyingi sana kuliko nchi yoyote kusini mwa jangwa la sahara ukiondoa Afrika kusini. Hata wale wanaotetea na kusifia vyama vyao wanafanya hivyo kwa nidhamu ya woga tu mana wanajua wakionyesha misimamo yao waziwazi rungu la vyama vyao litawaponda vichwani mwao hivyo wanabaki wakisifia vyama vyao bila kupenda bali kwa unafiki kwa vile wanajua wanalambalamba chochote kutokana na vyama hivyo. Shime sasa tuukatae umasikini huu tulio nao wa viongozi.Sina haja ya kurudia maneno ambayo wananchi wengi wanayaongea viongozi kujilimbikizia mali na ubinfsi uliokithiri na kutowajali wananchi ambao wanazidi kumasikinika kila kukicha. Sasa viongozi wa aina hii ni wa kazi gani katika nchi? Wanaona starehe gani kwa kuongoza masikini. Sipendi hata kuongelea juu ya utajiri uliopo katika nchi hii ambao wote uko mikononi mwa viongozi bila kujali kugawia wananchi wanachostahiki. Najua iko siku kila aliechukua mali ya wananchi atairudisha kwa wananchi apende asipende Mungu hapendi dhuluma. Amini nawaambia siku inakuja haki itatendeka kabla ya kuisha kwa ulimwengu huu.Wananchi tukiamua tunaweza. Wakati sasa umefika wa kuamua tena tumechelewa sana sio kupiga kelele kila siku. Watu husema kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Tukijatahamaki maji yote yatakuwa yamekwisha kisimani. Mwenye masikio asikie, na mwenye macho aone
Ni mimi mpenda haki
Tanga.Tanzania
Tags:
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
chama baby |
| 5 |
Sili Silali |
| 6 |
IL-YA |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
mohd nasser |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Hellen Attarsingh Gupta |
Sili Silali liked GLOBAL's blog post PSI YATOA SEMINA YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KATIKA MABAA NA VILABU YA POMBE JIJINI MBEYA
Saleh Jadid Saleh commented on IL-YA's blog post Dubai:House girl,achanganya mkojo wake na chakula cha mwajiri wake!.Huko Singapore nako wembe ni ule ule!
IL-YA replied to Hussein Marandu's discussion UMMA WA KIISLAM NA KUJENGA JUU YA MAKABURI:Kwanini ukweli huu unafichwa? in the group UKUMBI WA KISLAMU
chiya left a comment for Jazihina Jaziu
arthur moore commented on IL-YA's blog post Dubai:House girl,achanganya mkojo wake na chakula cha mwajiri wake!.Huko Singapore nako wembe ni ule ule!
