Ni matumaini yangu kuw hamjambo, poleni na majukumu mengi ya ujenzi wa Taifa letu.
Ikiwa ni mara yangu ya tatu tu kuweka mjadala humu, leo nimekuja na jambo ambalo binafsi kama mtumishi wa serikali limenigusa sana tu. ni kuhusu kodi kubwa tunazotozwa watumishi. nitachukulia mfano wa mtumishi anayelipwa laki sita kwa mwezi kodi anayotozwa inafikia kiasi cha chilingi 97,000/= kila mwezi.kwa mwaka mmoja ni 1,164,000/=
binafsi nilikaa na kuchambua kodi zingine za nyongeza anazokatwa huyu mtu nikaona ya kuwa tunibiwa bila ya kujua tukiwa tunachekela mwizi wetu.
Hebu kwa haraka tu niwajuze hili.
Umeshalipa laki moja kama kodi ya PAYE bado ukienda dukani kuna 20% VAT
 kwa kila unachonunua.
Ukipanga nyumba napo kuna kodi ya pango ambayo imeingizwa hivi kaibuni, ukiendesha gari lako kuna kodi kubwa tu unatakuwa kulipia pale TRA, ukisafiri vilevile,
ukiangalia mbunge anayelipwa milioni 12 kwamwezi hakatwi kodi hata senti, bado huyu ana marupurupu mengi tu. akimaliza muda wake anapewa milioni 40, kwa muda wa miaka5 tu. na kipindi kijacho itakuwa hivyo.na wengine ndo kama tunavyowaona kwena kupiga meza na kulala mjengoni.
Serikali yetu inge angalia utaratibu wa kila mfanyakazi akawa na TIN namba yake anapofika dukani anaonyesha na bei anayouziwa inakuwa bila VAT . ama ungeandaliwa utaratibu wa kompyuta zikafanya kazi kama hii,.

Views: 5

Reply to This

Replies to This Discussion

helow bro,unayosema ni kweli kabisa,na ukizingatia hasa katika sekta watu binafsi wanaokuja kuekeza.JAMANI YAANI UONEVU MTUPU WAKUBWA ZETU WANAO TUFANYI(WALOSHIKA MADARAKA KTK NCHI)yaani mtu anatoka nchini kwake na kuja kuchuma kwetu na pia kuchukuwa nguvu za mwananchi na pia kwa mshahara mdogo na hapohapo serekali pia anachukua kodi.hawatizami nguvu za mtanzania na mali zetu.jee ni haki?eti tuna vyama vya kututetea kama tuico na kadhali ila watu hawa mbona hawafatilii?mishahara mibovu,matusi ya kunyanyaswa na kazi nyingi mbali ya makubaliano na hata over time au lunch hupewi na tunafanya kwakuangalia hatuna pa kwenda na tuna familiya inatusubiri,jee jamani tunasema nchi yetu ina amani,ni kweli ina amani au tuna uwawa huku tunajiona?watu wanagombea viti eti kura(mi simpi mtu kula maana sio kura ni kula)inanitia hasira sana nikizingatia nilivyokuwa uwarabuni natuwa kama mtumishi na mwenye nchi akikuona umeekaa hospitali na hakuna siti ndugu yangu utaamka umpishe yeye akae si kwake?ila sisi mkaribishe mgeni ili atutawale na anakuwa na power kuliko wewe mwananchi.jee ni haki/ama kweli viongozi wanasahau majukumu yao na hawakumbuki kama madaraka ya ukubwa ni dhamana kwa mungu
tatizo watanzania tunajua haki zetu lakini hatuna wa kutupa haki kwani kiukweli kuna vitu pia hatufanyi uchunguzi wa kina si kila mtu anaponunua kitu ahjui kuwa kuna bei ya vat ila kwa kuwa kitu hicho kila mtu anahitaji hana jinsi ya kukataa na viongozi nao hawalioni hili swala kwani wanachoangalia ni maslahi yao Waswahili husema mvuta kamba huvutia upande wake.tunahitaji kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika uchaguzi na wale wanaozembea tuwe tayari kuwabainisha.na kinachotugharimu zaidi ni woga wa kumwambia mtu ukweli tunakuwa tayari kumwamini kiongozi kwa haraka bila kufikiri kwa kina
Ni kweli kabisa lzm serikali iangalie hili suala la kodi linaumiza sana.
Kweli kabisa unajua tunalipa kodi mara mbili wafanyakazi?!
Serikali inahitaji kuchakachua system zake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, la sivyo kuna siku tutalipia hadi pumzi tuvutayo.

Mwenzetu umenena! ukiacha PAYEE bado kuna ada za vyama vya wafanyakazi, jamani hivi navyo vinakata pesa yetu nyingi sana, hili nalo litazamwe kwa kina. Nimeona wenzetu wa Ghana, mfanyakazi anaponunua kitu / bidhaa dukani anaonesha ID yake anauziwa hitaji lake bila kodi, hii ni kwa sababu anahesabiwa kuwa alishalipa kodi. Hapa kwetu kodi tunayokatwa haileti mantiki maana kila kitu tunalipia kodi, labda ubahatishe kununua gari mara moja kwa miaka minne ndo utapata msamaha.

UKIYAWAZA SANA HAYA UNAWEZA KUJIKUTA UNALIA MWENYEWE CHUMBANI. MAUMIVU YA MFANYAKAZI NI MAKALI. KODI YA MFANYABIASHARA AKIFIKISHA MILLIONI 10 KWA MWAKA UJUE HIYO NI BONGE LA BIASHARA INAYOINGIZA MAMILLIONI KWA MWEZI, KUMBE KWA MFANYAKAZI, NI MSHAHARA ULIO CHINI YA MILLIONI MOJA. CHA AJABU SASA, PALE UNAPOFANYA KAZI KWA MWEKEZAJI ALIYESAMEHEWA KODI, WEWE NA TUSENTI TWAKO BADO WANAKUFULIGISA NA BONGE LA KODI, SASA HII NI NINI? KICHEKESHO ZAIDI NI KUWA MSAMAHA WA KODI NI KWA MWEKEZAJI MKUBWA WA NJE TU, WA NDANI HATA AWE NA MTAJI KIASI GANI NI KUKANDAMIZA TU!! JAMANI, HIVI KUUFURAHIA UHURU WAKO MPAKA WOTE TUWE BUNGENI?  KWELI NDIYO MAANA KILA MTU ANAOTA KUWA MBUNGE AISEE!

Mi nafikiri serikali haijaamua kulifanyia kazi hili. Lakini serikali inayojali watu wake inapaswa kutokaa kimya. Wakati umefika wa serikali yetu kuliangalia suala hili kwa upya kwani baadhi ya wafanyakazi wanalipa kodi kubwa hata kuliko wafanyabiashara ambao kipato cha mwezi ni zaidi ya mshahara wake mara tano. kwenye kodi haswa PAYE wafanyakazi wengi ni kweli wanadhulumiwa kabisa na hivyo kushindwa kujiletea mandeleo na kufikia malengo waliokusudia.

KODI TUNAYOWEKEWA NA SERIKALI NI KUBWA MNO,HUU NI UONEVU NA WIZI

matatizo hii its happen to alot people even kaka yangu anafanya kazi monday to sunday kwamshara mdogo . kuna wengi wanahangaika just to supporting there family.. its hard and goverment wanatakiwa wabadilishe ..

KWELI KABISA  WAFANYAKAZI TUNAIBIWA

RSS

ADVERTISEMENT

TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

Profile Icon
kalisa bruno taifa commented on Dongonyo Juniour's photo
aaaaaaaaaaaaa hata million pound unaweza kutoa
23 minutes ago
Profile Icon
Profile Icon
Profile IconProfile Icon
sophy and mency mgl are now friends 32 minutes ago
Profile Icon
nance liked GLOBAL's blog post 'Shilole aifungukia stori yake ya kubakwa' 40 minutes ago
Profile Icon
mency mgl left a comment for neema molleli
I LIKE YA PROFILE 
55 minutes ago
Profile Icon
mency mgl commented on mency mgl's photo
Hunizidi mimi FURAHA, yani nawapenda sana wote wawili
1 hour ago
Profile Icon
18 blog posts by GLOBAL were featured 1 hour ago
Profile Icon
Blog posts by GLOBAL 1 hour ago
Profile Icon
julius manning commented on GLOBAL's blog post 'KATUNI...'
atampa kila kitu !!!!! sijamwelewa kabisa !!
1 hour ago
Profile Icon
julius manning commented on GLOBAL's blog post 'Uwoya, Wema, Kajala wanatumia dozi'
kichwa cha habari kina uzito mkubwa mi nilifikri wana dozi ya Mzee wa Loliondo
1 hour ago
Profile Icon
mwachali.rogers commented on GLOBAL's blog post 'Caf yaitosa barua ya Yanga SC'
Yanga acheni uoga mnadhani hata caf wakikubali ichezwe 1 mnafikiri itafanyika hapa bongo? Bora…
1 hour ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service