Tanzania hakuna wanasiasa,wote njaa tu na ulevi wa sifa ndo vinawasumbua! mwanasiasa ni mtu wa kuona mbali,sasa wenzangu na mimi wanataka kuingia madarakani au wapo madarakani kwa visera vyao vya miaka mitano mitano,tutafika wapi. Vi-sera vyao ukivisoma kwanza sio representative kwa mawazo na mahitaji ya watanzania wote, pili viko kama bajeti za kuendeshea kay moja tu na sio taifa!
Na ndo maana wanatuingiza katika mikataba ya kihuni isiyokuwa na tija kwa taifa,sababu hawaoni mbali,pia uwezo wao wa kufikiri na kuongoza ni wa kiwango cha familia tu na sio taifa!
Linapotokea tatizo hukurupuka na kutafuta shortcut kuficha tatizo,matokeo yake ndio hayo ya kuilipa DOWANS pesa ambazo tunazihitaji sana katika kipindi hiki,au yale ya kuanzisha bodi ya mikopo bila kujua itafanya kazi gani,wala kujua ugumu wa kazi ulivyo,wanakaa na kula pesa tu katika vikao,wakiwaacha vijana wanahangaika na masomo bila hizo pesa walizo sema watawapa. Hii ni aibu sana kwa taifa lenye miongo kadhaa tangu uhuru!
Umasikini tunaotakiwa kupigana nao kwa sasa,sio wa mali/pesa bali ni wa kukosa viongozi wenye maono (Vision) ambao ndio kimekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya taifa hili.
Adui mkubwa wa watanzania sasa sio Maradhi,umasikini na ujinga,kama alivyosema Mwl JK Nyerere, bali ni hao wapiga porojo wanaojiita viongozi/wanasiasa na hali uongozi hawaujui na hata hawajui siasa.
Tanzania sio masikini,kinachokosekana ni vipaumbele,hakuna hata siku moja,tukaweza kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja,matokeo yake yatakuwa duni kwa sababu kutakuwa na divided attentions ambazo zitapelekea kupungua kwa ufanisi kwa kila kitu tunachogusa kufanya kama taifa,ambayo ni upotezaji wa rasili mali kama tunavyoona sasa!
Ukweli ni kwamba rasili mali kubwa kwa nchi yoyote ni watu,ndo maana nchi kama Canada na zingine za ulaya wanashawishi watu wahamie huko wapewe uraia ili watumike katika kujenga uchumi, je katika hili tanzania tutasema ni masikini na hali tuko 40milion. Rasili mali nyingine ni ardhi, je katika hili tutajitetea vipi? Kama kweli sio fikra mgando za hao wanaojiita viongozi wetu!
Aaaaaaaaagh! inaudhi bwana,hebu tufikirie kidogo nje ya box ili twende mbele. Sio lazima kuiga kila kitu kutoka nje ili kuendelea, wako wasomi watu hebu tuwatumie.
Viongozi wa tanzania wasikilizeni wananchi,na hasa hao wasomi na wenye uelewa,wanayo majibu sahihi ya matatizo yao/yetu. Na sio nyie kila kukicha mnajifungia kwenye vikao mkidhani mnaweza kuleta maendeleo ya tanzania kwa vikao na posho mnazojilipa! Na wala sio safari zenu za nje za kila siku ambazo kiukweli hazina faida kwa mtanzania wa kawaida.
Enyi viongozi,vueni hiyo miwani mlo vaa,manake mnakotupeleka kuna bonde kubwa,tutatumbukia humo na hatutapata wa kututoa,acheni kujifanya viziwi.
Ndimi Mkaapembeni!
Tags:
Permalink Reply by Sebastian Salatiel Shemhilu on March 21, 2011 at 12:24pm
Permalink Reply by DINA FLAMINGO on March 22, 2011 at 3:00am
Permalink Reply by maxmilian Annaely Arasululu on March 23, 2011 at 11:28am
Permalink Reply by jeff lamchina on March 23, 2011 at 1:57pm kaka umenena ukweli toka uvunguni mwa roho yako.
That is the real situation surrounding us!
NOW tuonyeshe mfano basi kaka ili wakufuate!
Permalink Reply by suleiman haji on March 23, 2011 at 5:09pm Me nadhani si tu kwa Tanzania but for all African countries. sisi siku zote tutakuwa wasemaji tu jamani mtendaji wa haya mambo ni nani? kwanini tuwe hivi? me na wewe mwezangu tutaongea tu but hakuna hatua yoyote. Ndio viongozi ambayo hakika ndio hao wanasiasa ni wahudumu wazuri wa ushauri nasaha kwanini Wizara husika, NGOs and Taasisi nyengine zinazodai kutoa huduma za ushauri nasaha kwa watu wa VVU and AID wasiwatumia wanasiasa kwakuwa wao ndio wenye taaluma ya kuyarejesha matumaini kwa waliopoteza ,hii ni kwasababu sisi sote sio siri watawala waliopo hatuwataki but when uchaguzi ukikaribia sote tunarejelea yale yale yanayotukandamiza just for kitu kidogo, kitenge, promotion za kupandishwa kwenye jukwaa, etc. me nawaambia Waafrika wezangu nilazima tuondowe ule ukiritimba wa nafsi zetu kwa kila mmoja kumjali mwezake finish. i believe if every one atakuwa na high % of concern for other people of different group will no suffer as to day we do. lack of concern for the people by each other is the largest problem which linasababisha mwanachi na mwanasiasa kuwa firimbi( porojo tu)
more discussion watanzania
Permalink Reply by Mohammed Mzee Mtahu on March 23, 2011 at 7:42pm Kwa hakika hoja zako zina mashiko ingawa zina mzizimo.Kwa kweli hadi leo tujadilipo hoja hii ya wanasiasa wetu bado ni wale ambao wameweka maslahi yao mbele zaidi kuliko maendeleo ya Taifa.Hata hivyo mfumo wetu wa utawala bado ni tatizo.Mimi nadhani ipo haja kubwa ya kuangalia kwa makini mfumo wetu wa utwala.Siasa ni mbinu tu ya kutawala na siyo mfumo wa utawala.
Kundi lolote la watu wenye msimamo, itikadi na mtazamo wa aina moja wakifikia mahali wakajiona wao ndiyo wao lazima itokee kama itokeavyo nchini kwetu hivi sasa. Kinachotakiwa kufanywa si kugawanyika ila kuunganika ili kuijenga nchi.Kwa bahati mbaya kabisa wasomi ndiyo hao wapiga porojo kama ulivyowaita. kwani wasomi ni nani.Miongoni mwa viongozi wetu wapo maprofesa, madaktari na wale wenye digrii kwani si ndo hao waimalizao nchi.HAKUNA CHA USOMI WALA NINI, KINACHOTAKIWA NI UZALENDO.Kwanza wasomi hawana uwezo wa kuongoza. Wao ni wataalam tu wameacha fani zao wanasumbua watu na kudidimizaa nchi.
Permalink Reply by julius dominic on March 23, 2011 at 9:32pm
Permalink Reply by rf on March 23, 2011 at 9:53pm
Permalink Reply by suleiman swalehe on March 24, 2011 at 4:27pm
Permalink Reply by FARAJI MOHAMED on March 24, 2011 at 8:22am
Permalink Reply by mlelwa thomas on March 24, 2011 at 10:47am
Permalink Reply by Delly peter mandah on March 24, 2011 at 12:02pm | 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
LJH_3 |
| 5 |
hope |
| 6 |
Tatu Majaliwa |
| 7 |
mayalilwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Matilanga Lukingita |
| 10 |
Mishy chunga |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE yesterday. 27 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
© 2013 Created by Global Publishers.



