MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake ya Azam, pasipo makubaliano na yeye mwenyewe. Je, kitendo hiki ni cha kiungwana na kinalijenga soka letu? TOA MAONI YAKO TAFADHALI...

Tags: SOKA

Views: 3080

Reply to This

Replies to This Discussion

SI HALALI, ANAWEZA ASIFUNGE MABAO AU AKACHEZA CHINI YA KIWANGO

hii siyo halali hata kidogo na inatoa picha kwamba timu hizi mbili zina ushirikiano wa hatari kwa soka la tanzania.wenye akili tulishajua mapema kwani tangazo la kumuuza ngassa lilitoka wakati simba wameshapeleka ofa,halafu dau la simba likatangazwa baada ya yanga kupeleka ofa.halafu kama ni kweli walikuwa wanahitaji timu yenye dau kubwa mbona biashara yenyewe imefanyika haraka haraka,siku tatu tu,hii haingii akilini.Lakini ni hao simba waliokuwa wanamzomea ngassa na kumtuhumu kucheza kinazi,hamuoni kwamba maisha ya ngassa sasa yamo hatarini zaidi kwani kila atakachokifanya kule simba kitaangaliwa kwa historia yake na sio kibinadamu kwamba kuna siku hatakuwa fiti na kucheza chini ya kiwango

c halali hat kidogo, na nina waswas na akili za viongoz wa simba,ngasa kwa anachoshutumiwa azam n usaliti kwa azam juu ya mapenz na yanga sasa cjui kwa akili ndogo kabsa je simba ndo itampotezea mapenz na yanga? nafikri wanajua wazi hayupo tayari kucheza cmba ko wanamkomesha na kama ndo mapinduz ambayo wadau wamekuwa wakiisifu azam imeyafanya kwa hili nafkiri linawaharibia xan na cshangai ikaja kuwa kam moro united ilivotiksa na sasa kushnei manake nawaona wamelewa xan cfa tena mapema

Rehema Ahmed,

Kitendo hicho si uungwana hata kidogo. AZAM wanajichimbia kaburi lao wenyewe. 

huu ni utumwa mambo leo. kwanini afanyiwe hivvo

kiu kweli sio halali kwa sababu wakati walipo mtaka kumchukua yanga walienda na wakaa na wakaongea na mchezaji mwenyewe akalidhia kwahiyo kwanini sasahivi wamuuzi ovyo kwa hiyo hilo si halali wakae nakuongea na mchezaji mwenyewe haridhie azam wamekosea

KWA MTAZAMO WAO WANAONA NI SAHIHI ILA KWA MTAZAMO WA KIMICHEZO SIO SAHIHI HATA KIDOOGO KWA HII NI SAWA NA KUPIGA KISIKI KWA MAKUSUDI!!!

wao wanaona ni sawa kumchukua lakini wanatakiwa wajue kuwa ni kosa ni kubwa sana kimichezo,
wao wanaona ni sawa kumchukua lakini wanatakiwa wajue kuwa ni kosa ni kubwa sana kimichezo,
hivi ingekuwa wao ndo wamefanyiwa hivyo ingekuwaje au wangejisikiaje kiubinadamu tu, maana watakuja kutwangana halafu iwe tabu.

Mfungwa ni mfungwa tu hachagui gereza yeye ni mchezaji hawezi kuchagua mahali pa kuchez hataki aanzishe timu yake mbona hao yanga wamemdharau kwa kutoa dau dogo na sakata lake lilikuwa kabla ya twite tulia dogo cheza mpira ndio ajira yako hiyo achana na tabia za kitoto hawakutaki hao yeboyebo  wangekutaka wasingeona ubahili kutoa kitita kikubwa kwakoumefika kwenye klabu ya baba yako acha ujinga 

KWA KWELI HAWAKUTENDA HAKI LABDA WANGEMPELEKA YANGA

RSS

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

mjoanwee posted a status
6 minutes ago
rana posted a status
10 minutes ago
mjoanwee posted a status
16 minutes ago
rana posted a status
19 minutes ago
mjoanwee posted a status
23 minutes ago
mdsohel173 posted a status
24 minutes ago
mdsohel173 posted a status
25 minutes ago
misu babu posted a status
"[ESPN-TV] New Zealand vs Tonga live Rugby Video Coverage http://alturl.com/oyqpq"
28 minutes ago
misu babu posted a status
"[ESPN-TV] New Zealand vs Tonga live Rugby Video Coverage http://alturl.com/oyqpq"
29 minutes ago
mdsohel173 posted a status
30 minutes ago
mdsohel173 posted a status
30 minutes ago
misu babu posted a status
30 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }