Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban miaka sita tangu aingie Ikulu haelewi wajibu wake.

Hivi msomaji mpendwa wa blogu hii utamuelezeaje Jakaya Kikwete,Rais wetu,baada ya kumsikia akijitetea kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania kuwa "unyama wa hali ya juu uliofanywa na polisi huko Arusha,na kusababisha vifo vya Watanzania wasio hatia,ni BAHATI MBAYA"!!!

Yani Kikwete aliishiwa kabisa na cha kudanganya mpaka akakurupuka na excuse dhaifu kiasi hiki!Bahati mbaya kwa maana gani?Bahati mbaya IGP Said Mwema kutengua dakika za majeruhi ruhusa ya maandamano iliyotolewa na RPC wa Arusha?Bahati mbaya polisi kuachana na jukumu la kusindikiza maandamano ya amani na badala yake kuanza kuwaadhibu wananchi wasio na hatia ambao "kosa" lao lilikuwa kutumia haki yao ya kikatiba kuandamana kwa amani?Bahati mbaya kupuuza miito kutoka kada mbalimbali juu ya umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa umeya wa Arusha?Au bahati mbaya kwa risasi kutoka kwenye mitutu ya bunduki na hatimaye kutoa uhai wa Watanzania wasio na hatia?

Au Kikwete alikuwa anamaanisha kwamba unyama wa polisi wake dhidi ya wafuasi wa CUF walipoandamana,au vitendo vya udhalilishaji vya polisi hao dhidi ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki,au unyanyasaji uliozoeleka dhidi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kila wanapoandamana,ni BAHATI NZURI kwa vile hakuna aliyeuawa?

Nashindwa hata kuhisi mabalozi walipatwa na mawazo gani walipomsikia mkuu wa nchi anatoa kauli ya ajabu kiasi hicho.Nahisi kuna waliomhurumia kwa kijibebesha jukumu asiloweza.Hii inanikumbusha wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 (ambazo zilinikuta nikiwa huko nyumbani kwa miezi kadhaa).Kuna baadhi ya wajuzi wa siasa za Tanzania waliniambia kuwa Kikwete anaweza kushinda urais kwa vile ana timu ambayo iko tayari kufanya lolote kuhakikisha anapata ushindi LAKINI urais wake utakuwa kituko.Na kituko amekuwa.

Kuna watakaosema wa kulaumiwa ni washauri wake.Lakini hao watakuwa wamesahau kuwa alipoanguka Mwanza alitanabaisha kuwa huwa anapuuza ushauri wa washauri wake (ambapo tulielezwa walimshauri apumzike kabla ya kukumbwa na zahma hiyo).Sasa inawezekana kabisa kuwa hata kabla ya kuongea na mabalozi hao,washauri wake walimshauri kitu sensible cha kuongea lakini akapuuza.Au pengine waliona hakuna haja ya kumshauri mtu ambaye ni "haambiliki".

Lakini tukiweka kando excuse hiyo ya kitoto iliyotolewa na mtu tuliyemkabidhi jukumu la kutuongoza Watanzania takriban milioni 50,ukweli kwamba Kikwete amediriki kujiumauma kwa mabalozi unapigia mstari ushauri niliotoa kwenye makala yangu iliyopita.Katika makala hiyo niliwashauri Watanzania wanaoishi katika nchi wafadhili wa Tanzania kuwasiliana na wabunge/wawakilishi wao na kuwafahamisha udikteta wa Kikwete,kisha kuwaomba wafikishe kilio cha Watanzania kwa serikali za wafadhili hao.Kikwete amelazimika kuokoteza excuses kwa vile anatambua bayana kuwa ni lazima awapoze wafadhili kwani mchango wa wafadhili hao ni muhimu sana kwa ustawi wa taifa letu.Ni muhimu zaidi kwa ustawi wa Kikwete na serikali yake inayosifika kwa matumizi ya anasa yanayozidi mapato.Wafadhili wakiamua kusitisha misaada,serikali itaanguka within months if not weeks.Lakini idea yangu ya kufikisha ujumbe kwa nchi wafadhili haikulenga kuwashawishi wasitishe misaada bali naamini wao wanaweza kumbana dikteta huyu aanze kuheshimu haki za binadamu.

Na kuthibitisha kuwa Kikwete alikuwa anawazuga mabalozi hao,gazeti la Tanzania Daima lina habari kuwa jeshi la polisi limezuia maandamano ya amani huko Songea yaliyoandaliwa na Chadema kupinga ufisadi katika sekta ya kilimo. Huu ni uthibitisho tosha kuwa unyanyasaji wa raia wasio na hatia na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi sio suala la BAHATI MBAYA kama anavyozuga Kikwete.Ni utekelezaji wa maagizo ya serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Kikwete huyohuyo.

Hivi Kikwete ameshindwa angalau kuwatosa Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha,IGP Mwema na RPC wa Arusha kuwa "mbuzi wa kafara" ali mradi imsaidie kudanganya kuwa yeye hahusiki na maagizo yaliyopeleka polisi kuua.Hawezi kuwatosa kwa vile ni kiongozi anayeendekeza ushkaji.Sasa kama familia haiwezi kuongozwa kishkaji,nchi ikiongozwa kwa mtindo huo inakuwaje?

Na kuna kila dalili kuwa hivi sasa Kikwete anaongoza nchi na CCM yake kwa mtindo wa "bora liende".Hebu angalia jinsi ishu ya fidia kwa Dowans inavyoonyesha mparaganyiko kwenye kabineti ya Kikwete.Wakati Waziri William Ngeleja anatweta kuwakikishia mafisadi wa Dowans kuwa lazima walipwe kwa utapeli wao,Waziri Samuel Sitta anatangaza hadharani kuwa kuwalipa Dowans ni jambo la hatari.Uwajibikaji wa pamoja Kikwete's cabinet style!Huko CCM,Katibu wa chama hicho mkoani Arusha,Mary Chatanda anawawakia viongozi wa dini akiwataka wavue majoho yao wajiunge na siasa badala ya kukemea maovu (mpuuzi huyu anakosa adabu hata kwa Watumishi wa Mungu!).Kwa upande mwingine,Katibu Mkuu wa chama hicho,Yusuph Makamba,anadai kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake including viongozi wa dini.Na yote hayo yanatokea huku yakiweka kivuli kwenye tukio la kihistoria la diwani wa CCM kujiunga na Chadema.Tukio hili linapaswa kuchukuliwa kama ugonjwa nyemelezi kwa mwathirika wa ukimwi: linaashiria mwanzo wa mwisho wa CCM.

NIMALIZIE KWA KUKUMBUSHIA WITO WANGU KWA WATANZANIA WENZANGU WANAOISHI NCHI ZA WAFADHILI WA TANZANIA.KUWA MBALI NA NYUMBANI ISIWE SABABU KWETU KUSHINDWA KUSAIDIA UPATIKANAJI WA UHURU WA PILI WA TANZANIA (wa kwanza ulikuwa wa kumwondoa mkoloni,wa pili ni wa kuondoa udhalimu,ufisadi,ubabaishaji,unyanyasaji,ukiukwaji haki za binadamu,udikteta na kila baya unalofahamu).TUWASILIANE NA WABUNGE/WAWAKILISHI KATIKA MAENEO TUNAYOISHI NA KUWAOMBA WATUFIKISHIE KWA SERIKALI ZAO VILIO VYA WATANZANIA WENZETU WANAONYANYASIKA KWA KILA HALI CHINI YA UTAWALA WA KIKWETE NA CCM YAKE

http://chahali.blogspot.com/2011/01/kauli-ya-jk-kuwa-mauaji-ya-arus...

Views: 5032

Reply to This

Replies to This Discussion

Ninahakika miaka 8 iliyopita usingeweza kuandika ulichoandika otherwise watoto wako wangefananishwa na YATIMA. Ndugu, jamaa na marafiki wasingejua ulikopotelea. Hebu jaribu kupunguza uvivu wa kufikiri kwanini hukumwandika MKAPA aliyouwa watu zaid ya mia UNAMWANDIKA JK aliyeua 3, ulishawahi kujiuliza unakiasi gani cha ujinga? Jaribu ku-recall miaka 8 iliyopita kuna m2 angethubutu kusema nchi hii haitawaliki na bado aendee kupiga kelele? BINAFSI ningepata nafasi yakumkosoa  JK, Ningesema hivii!! Umefanya kosa kubwa kuwapa wananchi uhuru wasiowastahili
huyu jamaa sijui hata anaongea nini! kweli kaka godshine mkumbushe kipindi cha mkapa, inawezekana kijana ndo kaanza kukua ss. halafu anakurupuka tu kuongea nonsense, angekuwa yeye ndo kikwete angechukua jukumu gani hapo. unajua, tusikalie kulaumu tu, pia tujiulize ingekuwa mm ndo kikwete, ningefanya nn kwa situation ile. au unaaka kutuletea mambo ya siasa za ajabu! tatizo kikwete ni mpole sana na ndo maana watu wenye mawazo dhaifu hawaoni hata anachokifanya.

taratibu mkuu

Hakuna cha kusema Jk ni mpole!hajui afanye nini ama anashindwa kuamua afanye nini!mana na yeye inaonesha ni mhusika wa kila ki2!kama angekuwa si mhusika angetoa kauli au kufanya uamuzi mgumu.Tatizo serikali yake imekaa kishikaji tu!anawalinda!Kumbuka uongozi wa Mkapa hata infletion ilikuwa chini,hapakuwa na Mgawo wa umeme,hapakuwa na tatizo la mafuta!Bwana msilolonge bila kufikiria!UKWELI NI KWAMBA KIKWETE SI KIONGOZI!KUMBUKA MANENO YA MWL.WAKATI KIKWETE ALIPOGOMBEA KWA MARA YA KWANZA.

wewe ni mjinga ujuhi unachokisema

kwa hiyo wewe ulitaka awafufue? kwanza kuwa na uhakika kwa mambo unayoandika, ulitaka watu wengi waumie kwa sababu ya upumbavu wa watu wachache? acha porojo zako tumechoka na maandamano ya uchochezi, tunataka maandamano yenye manufaa. ungetumia busara kuwaomba viongozi wako wa chadema waombe vibali kwa serikali wakusanye mafundi wajenzi kujenga walau nyumba za maskini na wasiojiweza, kutumia nguvu kazi katika maeneo wanayotoka kuchimba visima wananchi wajipatie maji au hata kuandamana kwenda mashambani kulima wajipatie chakula, ili wavutie wanachi kuwapigia kura 2015.

KWA KWELI WAPINZANI MNATUCHANGANYA MKIPEWA NAFASI MNASHINDWA KUTIMIZA AHADI ZENU MNABAKIA KUJINUFAISHA NYINYI TU NA FAMILIA ZENU. BORA CHAMA TAWALA KIENDELEE NA KAZI MAANA WAO KAZI YAO NZURI ISIPOKUWA WATU BINAFSI TENA WACHACHE AMBAO TUNAWAMUDU ILA WAPINZANI WAPO KIMASLAHI ZAIDI HAMNA LOLOTE MSITUDANGANYE HAPA TUKAINGIA VITANI KAMA SOMALIA ACHA TUFURAHIE UHURU NA AMANI  YETU HATA KAMA MASKINI. UWEZO WA CHAMA TAWALA KUIWEKA NCHI SALAMA KWA MUDA WOTE HUU WA MIAKA 50 SI KITU KIDIGO NYIE WAPINZANI, BORA MASKINI HURU KULIKO TAJIRI MTUMWAAAAA.

Hata ww ni muuaji!!!!! utamtukanaje kiongozi wako na bado anakuongoza? Wewe ni chadema acha ujinga unafki. kawadanganye wachaga!!!!!

kuna usemi usemao INZI MKOROFI HUINGIA NA MAITI HADI KABURINI  WAJINGA NDIYO WALIWAO. nafikiri hapa ni hoja ndizo zinazotakiwa lakini matusi na kejeli zina sababu gani hapa??!!!!!

HUYO NI CHANGU DOA TU,NI KAMA WALE WANAO JIUZA PALE OHIO

INAONEKANA ALIEANDIKA HIVI NI MWANASIASA ANAEEGAMIA UPANDE FULANI! NA NDO MANA HAKUWEKA JINA!! NA MANENO YAKE NI UCHOCHEZI WA VITA!!!!

Kikwete alikimbilia tu Ikulu bila kujua Ikulu anaenda kufanya nini,yafaa akaogopwa kama ukoma!

RSS

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }