HIVI KWELI VIONGOZI WETU WANA UCHUNGU NA WANANCHI WANAOSAFIRI KUPITIA RELI YA KATI?

Leo asubuhi kwenye taarifa ya habari kupitia television ya Taifa niliona kitu cha ajabu,pale nilipoona mpaka watoto wanahojiwa taabu wanayopata kupitia kukwama kwa safari yao kwa njia ya treni kwa mvua zinazoenelea kunyesha sasa,daraja la treni limeanza kuzama na hivyo kupelekea safari za treni kupitia njia hiyo kusimamishwa!!! kinachoniuma hapa ni ile hali ya wananchi kuendelea kuibiwa na kulala njaa huku wakingoja serikali iwaletee mabasi ya kuwanasua au kuwasafirisha kutoka hapo walipokwama.Jamani ungeona mambo yalivyokuwa mngeguswa sana...nashauri serikali kuwa makini au kufanyia uchunguzi barabara na reli hasa kipindi hiki cha mvua.NI HAYO TUU KWA LEO

Views: 2402

Reply to This

Replies to This Discussion

Tatizo ni lile lile, fikra mgando kwamba kila kitu lazima aje mwekezaji ndo mambo yaende,ona sasa yanayotokea. Mwekezaji kapewa hajali hata kufanya survey kuweza ku-anticipate ni wapi panaweza kutokea tatizo katika mfumo mzima wa reli.

Mwekezaji mara zote ana lengo moja tu akilini,kutengeneza faida na sio kujali na kuhakikisha miundo mbinu iko sawa.

Hivi shida yetu siku hizi nini jamani! mbona mkoloni aliwatumia babu zetu kiujenga hiyo reli ambayo tunatumia hadi sasa,sisi tunashindwa nini kama sio kithibitisho kuwa kuna matatizo ya kimaono kwa viongozi wetu.

Leo ni mvua, kesho itakuwa ni moto na wala hakuna hata hatua zinachukuliwa kumhakikishia msafiri wa hiyo reli kuwa likitokea la kutokea kua maandalizi ya kutatua tatizo haraka!

Kama mkoloni aliweza sisi tunashindwa nini kujenga nyumba yetu wenyewe katika kipindi hiki tunasema tuko huru na tekinolojia inatusaidia?

Mimi naona kuna shida hapo ya umbali kati ya wanaojiita viongozi na wanachi kufikia kiasi cha wao kushindwa kuwashawishi watu kufanya jambo kwa manufaa ya taifa zima. Na ukiona hivyo ujue tunakoelekea sio kwema sana.

Mungu ibariki Tanzania.

hahahaha du kaka umesahau ule usemi usemao kila mtu anakula kutokana na ulefu wa kamba yake. sahau hayo hakuna atakae jali.

WAKINA JAKAYA KIKWETE WANATAKA KURA TU HAKUNA KINACHOFANYIKA

 

Mwisho wa matatizo ya reli ni 80% kuibinafsha, kuwapa watu bunafsi walimbike kwenye shirika hilo. Kwea njia hii ulaji na uzorotaji utakomeshwa.... Kwa sababu iwapo watu binafsi watakuwa na hisa katika shirika hili watakuwa makini kuangalia kwamba hawaibiwi ndo maana wenzetu vitu vyao vina endlea. Chukuwa mfano Kenya Airways ina ubia na KLM ya Uholanzi.

Ndege ilikuwa inayomilikiwa na Serikali ya Kenya hadi Aprili 1995, na ili binafsishwa mwaka 1996, kuwa Shirika hilo kwa sasa ni la ushirikiano wa serikali na sekta binafsi. Mbia mkubwa ni KLM (26%), ikifuatiwa na Serikali ya Kenya, ambayo ina hisa 23% na wamiliki binafsikama  Nairobi Stock Exchange, Dar-es-Salaam Stock Exchange, na Uganda Securities Exchange.Kwa hali hii KLM hatokubali watu wale tu. wabia binafi watakuwa macho. Lakini Reli ya kati pamoja ma makampuni mengine yana milikiwa na serikali.... Hivi ni KULA KULA KULA KULA LAKINI usionwe na wengi wanaoshika ngazi za juu wanacheza kiwanja kimoja.

Na kama tutataka kubinafsisha basi ubinafsishaji uwe na watu wanao eleweka mfano mwaka  2007 mkataba  RITES Ltd. ya india kuendesha reli hiyo serikali ikawa na hisa ya 46%. Its just crazy watu wa serikalini. Kuna watu ambao hawana viwango na uwezo wa kundesha kampuni katika nchi yetu. Arrrrgh na pata vidonda vya tumbo!

 

Kwa nini wawe na uchungu wakati wenyewe wanatumia magari ya serekali. Sijui wanaotumia usafiri huo. Zingatia pia kupanda kwa bei ya vitu kwa mikoa ya Singida, shinyanga, Mwanza, Bukoba na kigoma ni kutokana na usafirishaji kuwa aaghari. Kama kweli viongozi wetu wangekuwa na uchungu na raia wenye hali duni wangetengeneza reli kurahisisha usafiri. Sasa kubwa ni kwamba viongozi wana biashara ya malori treni likipona watakosa biashara ndio maana hawapendi kutengeneza reli.

 

Kwa kuwa na mimi ni mhanga wa reli ya kati basi naona kuna umuhimu wa kuchangia mada hii. Ndugu yangu laiti ungeliona jinsi mchakato wa kujenga reli ya kati enzi hizo ungelijua ni jinsi gani watu waliohusika na ujenzi wa taifa wakati huo walivyokuwa commited. Mchakato ulikuwa too machenical ni sululu, jembe na kubeba reli begani. Leo tuna ma bull dozers, earth movers, crane za kubeba reli na utitiri wa vifaa ambavyo technolojia imetujalia  angalia yanayotokea. Sio kujenga reli tunashindwa kukarabatii!!! hebu tujiulize tatizo ni nini? Utaona dhahiri tatizo ni viongozi wanaojali maslahi yao zaidi kuliko maslaya taifa. Kwanza wameuza mashirika yetu bila kutushauri kwa kisingizio kuwa serikali inajitoa katika kufanya biashara. Lakini bei ya kujiuzua ni sawa na bure. Haya baada ya kuuza nini kinafuata ni kila mtu kujichotea. kwa kifupi ni kwamba reli ya kati na hasa ya kwenda kigoma ni bora watanzania mkasahau kwa sababu wakubwa wanasafiri kwa ndege na magari ya kifahari sisi kina kajamba nani tunalazimika kusafiri na treni na treni yenyewe si lolote si chochote unaweza kusafir kwa wiki mbili kutoka Dar kwenda Kigoma. Siku moja nilikuwa nasafiri nikitokea Kigoma kwenda Morogoro kwa mara ya kwanza nilishuhudia Treni ikiishiwa dizeli kama gari kweli nilishangaa sana. Nikasema kweli Tanzania imekwisha na Ukistajabu ya Musa Utaona ya firauni

 

SASA MLITAKA RAIS AFANYE NINI?

hawawajibishe wahucka

hapana mi naona hawana uchungu,na wala hawana mwelekeo wakuwa na uchungu hivyo basi watanzania ni wakati wa kufunguka hawa jamaa waachie dola 2015,ili wachukue wale wenye uchungu na wananchi wao,

Wanasiasa wapo wengi tu ila wanadhibitiwa, mnakumbuka zengwe alilopandikiziwa mzee wetu SALIM AHMED SALIM katika kinyang'anyiro cha nani ateuliwe kupitishwa katika nafasi ya kugombea nafasi ya urais toka ndani ya chama tawala mwaka 2005?

KUSEMA UKWELI INAHUZUNISHA KUONA VIONGOZI WETU HAWANA UCHUNGU NA WANANCHI WANAOSAFIRI KUPITIA RELI YA KATI.NAFIKIRI YOTE HII INATOKANA NA KWAMBA WAO SIO WAHANGA.NAWASHAURI WABADILIKE.

RSS

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

Polat Salla posted a status
23 seconds ago
sabuj posted a status
32 seconds ago
vitalia posted a status
51 seconds ago
kemeya posted a status
1 minute ago
Polat Salla posted a status
1 minute ago
kemeya posted a status
1 minute ago
jasuke emon posted a status
1 minute ago
War Tune posted a status
1 minute ago
kemeya posted a status
2 minutes ago
shyamal dhali posted a status
2 minutes ago
misu babu posted a status
2 minutes ago
shyamal dhali posted a status
3 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }