Photos

Loading…
  • Add Photos
  • View All

GLOBAL TV ONLINE

Members

ABDALLAH MRISHO

Videos

  • Add Videos
  • View All

Badge

Loading…
 

News Posts

BARUA PEPE ZA HILLARY CLINTON KUKAGULIWA

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 12:42pm 0 Comments

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bi. Hillary Clinton.

New York, Marekani

Maelfu ya kurasa za barua pepe (emails) binafsi za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bi. Hillary Clinton zilizotumwa kwa anuani binafsi ya Waziri huyo, zimewekwa wazi hii leo na idara za Usalama nchini humo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kuwa, kati ya barua pepe hizo, 150 kati yake ni zile zinazodaiwa kuwa na taarifa muhimu na za siri za serikali ya Marekani. Hata hivyo, Bi. Clinton mwenyewe amesema kuwa barua pepe hizo alizituma kimakosa, kwa kutumia anuani binafsi kwa shughuli rasmi za kiserikali.

Shirika la Ujasusi la Marekani FBI linachunguza ili kubaini kama ni kweli barua pepe…

MAMBO 10 YA KUEPUKA ILI SHERIA YA MITANDAO ISIKUPITIE

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 9:30am 0 Comments

Sheria ya mitandao inaanza kutumika rasmi tarehe 1 septemba 2015, haya mambo 10 muhimu ili sheria hii isikukamate

1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao

2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao.

3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp,Facebook,Youtube,Inst agram n.k

4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya…

SIMULIZI NZITO!

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 10:33am 0 CommentsMakongoro Oging’ na Haruni Sanchawa


HALI bado ya majonzi! Watu bado wanalia, hususan wakazi wa maeneo ya Buguruni, Ilala jijini Dar es Salaam kufuatia vifo vya watu tisa wa familia moja vilivyotokana na kuteketea kwa moto uliozuka saa tisa usiku wa Agosti 13, mwaka huu kwenye nyumba ya mzee Masoud Mattar Masoud ambaye siku hiyo ya tukio alikuwa kazini bandarini.

Muonekano wa…

MUME ALIVYOMUUA MKEWE KWA NYUNDO!

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 11:02am 0 Comments

Na Mohemed Shabani, Manyara

DUNIA inazidi kufikia ukingoni! Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Paulo Mahinda, 40, (pichani), mkazi wa Kijiji cha Ndaleta wilayani Kiteto, Manyara anatafutwa na jeshi la polisi wilayani hapa kwa madai ya kumuua mke wake, Mariam Samuel (45) hivi karibuni kwa kumpiga na nyundo kwenye paji la uso, pia kumjeruhi mtoto wake wa mwaka mmoja.

 Marehemu Mariam Samuel enzi za uhai wake.

Taarifa za awali kutoka kwa viongozi wa Kijiji cha Ndaleta zinasema kuwa, mwanamke huyo hakuwa tayari…

MGONJWA ALIA: SINA PESA, NAKUFA!

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 11:13am 0 Comments

Na Haruni Sanchawa

NASIKITISHA, Said Ndangaye Mwilu (57), mkazi wa Kimara Baruti, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam na mwenyeji wa Kilwa, Kijiji cha Kipatima, anaishi katika hali ya mateso makubwa baada ya sehemu ya mwili kuanzia kiunoni hadi miguu kupooza na kuibuka tundu kwenye kalio, magonjwa ambayo amedumu nayo kwa muda mwaka mzima.

Said Ndangaye Mwilu akiugulia.

Akizungumza na gazeti hili, mzee huyo amesema amekosa huduma za kimatibabu baada ya kukosa  shilingi milioni sita kwa ajili upasuaji.

Akisimulia zaidi mzee Mwilu alisema…

UCHAGUZI 2015, NI MWAKA WA TABU

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 10:30am 0 Comments

Mgombea urais wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Na Mwandishi Wetu

NDIYO lugha nyepesi kutamkika katika kipindi hiki ambacho nchi iko kwenye safari ya kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.Vyama vikubwa ni viwili, Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliomsimamisha Dk. John Magufuli na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliomsimamisha Edward Lowassa.

Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John…

WATANZANIA MUWE MAKINI KATIKA KUMPATA RAIS AJAYE

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 9:01am 0 Comments

 Rais Dk. Ali Mohamed Shein.

KWANZA tumsifu Mungu kwa kuendelea kuwapa moyo wa amani Watanzania, hili ni jambo muhimu kuliko kitu chochote hapa nchini.

Nianze kwa kusema kwamba kwa namna ambavyo vyama vya siasa vinaendesha mambo yao na demokrasia iliyomo ndani ya vyama hivyo ndivyo ambavyo vitaendesha nchi ikiwa mgombea urais atachaguliwa na wananchi kuongoza nchi.

Tusisahau pia kwamba madaraka hulevya; na hata kiongozi mzuri wakati hayupo kwenye madaraka hufaa kuchungwa anapokuwa kwenye madaraka, hivyo basi umakini mkubwa unahitajika kwa wananchi kuwachambua wagombea urais ili hatimaye kuchagua mtu makini.

Zanzibar vyama vimeteua wagombea, lakini wenye nguvu ni Rais Dk. Ali Mohamed Shein wa CCM na…

ELEWA UNDANI WA UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB)-2

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 9:00am 0 Comments

Naendelea kuelezea undani wa ugonjwa wa kifua kikuu ambapo leo nitazitaja dalili zake.

Dalili za kifua kikuu hutegemea sana ni mahali gani bakteria wa TB wanakuaw. Kwa kawaida bakteria wa kifua kikuu wanakuwa kwenye mapafu na kusababisha kifua kikuu cha mapafu.

Kifua kikuu cha mapafu kinaweza kusababisha kifua kikali kinachochukua zaidi ya wiki tatu, maumivu ya kifuani na kukohoa damu au makohozi.

Dalili nyingine za ugonjwa wa TB ni pamoja na udhaifu au uchovu, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula, baridi, homa na kutoka jasho usiku. Kifua kikuu tuli hakina dalili.

TIBA 

Kwa kawaida, mgonjwa wa kifua kikuu anatumia vidonge kila siku wakati wa matibabu yanayosimamiwa.

Ugonjwa wa kifua kikuu kikali unaweza kutibiwa kwa mchanganyiko wa antibiotics. Mchanganyiko…

FAHAMU MAZINGIRA RAFIKI YA KUJISOMEA

Posted by GLOBAL on September 1, 2015 at 10:53am 0 Comments

Kila kitu kina mazingira yake ya kuweza kukifanya kwa ufanisi ili kutoa matokeo yaliyokusudiwa kwa asilimia kubwa; vivyo hivyo zoezi la kujisomea kwa wanafunzi pia hupaswa kuandaliwa mazingira rafiki ili kufanya ubongo upokee mambo mengi kwa wakati mmoja na hatimaye kuweza kufaulu vizuri katika masomo yao.

Wanafunzi wengi hujisomea bila kujali mazingira ya kufanya hivyo jambo ambalo huwafanya washindwe kufaulu mitihani yao vizuri kwa kuwa ili mwanafunzi aweze kujisomea kwa tija hupaswa kusaidiwa na mazingira rafiki waliyojitengenezea yatakayomfanya awe makini kwenye masomo yake bila umakini wake kutekwa na mambo mengine.

Ukweli ni kwamba wanafunzi wengi siku hizi hujisomea kwa mtindo wa kupitisha macho tu kwa kuwa husoma huku akili zao zikiwa sehemu nyingine kutokana na mambo…

Advertisement

 
 
 

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }